Header Ads Widget

RAIS RUTO: WAGENI NDIO WANAOFADHILU MAANDAMANO DHIDI YA SERIKALI


Na, Matukio Daima App


Rais William Ruto sasa anashutumu mashirika ya kigeni ambayo hakuyataja kwa kufadhili maandamano nchi nzima dhidi ya utawala wake.

Akizungumza katika Kaunti ya Kajiado nchini Kenya alinukuliwa akisema: "Wale wanaojaribu kufanya mambo katika kupanga sijui wapi kupanga mambo ya nini, mimi nataka niwaambie Kenya ni taifa la kidemokrasia na hii ni nchi yetu na Kenya hatuhami," alisema.

Akijibu wito wa kumtaka kuondoka madarakani, unaoshinikizwa na vijana wa Gen z, Rais Ruto amesema Wakenya watapata fursa ya kutoa maoni yao katika Uchaguzi Mkuu ujao wa 2027.

Akisisitiza kuwa Kenya ni taifa la Kidemokrasia amesema hakuna njia za mkato na kwamba raia wanapaswa kusubiri uchaguzi ujao ili kuwachagua viongozi wapya.

“Kwa hiyo, hakuna haja ya kurejesha nyuma amani ya nchi, hakuna haja ya kutumia njia ya mkato, hakuna haja ya kutumia njia ya mkato. Wananchi hawa ni werevu na ndio wataamua vile Kenya itasonga mbele,” alisema.

Kwa muda wa wiki tatu zilizopita, vijana waandamanaji wanaojitambulisha kama Gen Z wamekuwa wakifanya maandamano makali kote nchini wakitaka pamoja na mambo mengine Rais Ruto ajiuzulu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI