MSHUKIWA WA MAUAJI KYLE CLIFFORD (26)
Mshukiwa anayesakwa juu ya shambulio lililosababisha vifo vya wanawake watatu amekamatwa.
Msako mkubwa wa polisi wa kumtafuta Kyle Clifford, 26, ulikamilika alipopatikana amejeruhiwa karibu na makaburi katika eneo la la London Kaskazini.
Waathiriwa, ambao walikuwa mke na binti wawili wa mchambuzi wa mbio za farasi wa BBC John Hunt, walishambuliwa nyumbani kwao huko Bushey, Hertfordshire.
Carol Hunt, 61, Hannah Hunt, 28, na Louise Hunt, 25, walipatikana wakiwa wamejeruhiwa vibaya nyumbani kwao majira ya saa moja jioni, Jumanne, na wote walifariki katika eneo la tukio hilo.
Mwanamke anayeifahamu familia hiyo aliwataja marehemu kuwa watu "wenye fadhila, urafiki na wapole" ambao "kila mara walitenga muda kwa ajili ya watu wengine".
Polisi walisema mshukiwa huyo, ambaye aliondoka jeshini miaka miwili iliyopita baada ya muda mfupi, alikuwa akipatiwa matibabu kutokana na majeraha yake, lakini "hakuna risasi iliyopigwa" na maafisa.
0 Comments