Na Matukio Daima App, Commoro
Kwa fahari kubwa, Mfalme Mohammed VI wa Morrocco amesheherekea miaka 25 ya mafanikio na changamoto za utawala wake katika aifa hilo.
Katika hotuba yake Jana Julai 30, 2024, Mfalme Mohammed IV amemshukuru Mungu kwa mafanikio ya kisiasa, taasisi, uchumi na masuala ya kijamii yaliyopatikana nchini humo katika kipindi cha utawala wake.
Mfalme ameangazia jitihada za kujenga utambulisho wa Taifa hilo, kuhakikisha umoja wa kijamii na kuimarisha nafasi ya Morrocco kimataifa.
Licha ya mafanikio hayo, Mfalme ameweka bayana changamoto zinazokabili Taifa hilo ikiwa ni pamoja na uhaba wa maji uliosababishwa na ukame na mabadiliko ya Tabianchi.
Amesisitiza umuhimu wa utawala bora, utekelezaji mzuri wa mradi wa usafirishaji wa maji, ujenzi wa mabwawa na mchakato wa kuondoa chumvi kwenye majichumvi kwa ajili ya matumizi ya binadamu.
Sambamba na hayo kupitia hotuba yake pia ameelezea msaada wa Morrocco kwa Palestina kwa kuelekeza misaada huko Gaza huku wakihamasisha maelewano ya pande mbili baina ya Palestina na Israel.
Mwishoni Mfalme ameyapongeza Majeshi ya Taifa hilo kwa kulinda umoja wa kitaifa na kuhakikisha usalama wa Taifa hilo.
0 Comments