Header Ads Widget

MBUNGE NDAKIDEMI AENDELEA NA ZIARA NA KUTEMBELEA KATA YA KIBOSHO MAGHARIBI



NA WILLIUM PAUL, MOSHI. 


MBUNGE wa Jimbo la  Moshi vijijini Profesa Patrick Ndakidemi ameendelea na ziara yake kwa kuitembelea Kata ya Kibosho Magharibi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo wa ujenzi wa Barabara ya Weruweru - Manushi - Kombo, Shule ya Sekondari Manushi, na Zahanati ya Kijiji Cha Manushi. 



Baadaye, Mbunge alizungumza kwenye mkutano wa hadhara na wananchi wa Kata ya Kibosho Magharibi katika Kijiji cha Umbwe Onana ambapo aliwapa taarifa ya utekelezaji wa majukumu katika jimbo kwa kipindi cha miaka minne ambapo kata hiyo imepokea kiasi cha Sh. bilioni 2,470,303,209.00.


Baadaye, Mbunge alisikiliza kero za wananchi, ambazo baadhi zilijibiwa na wataalamu wa Serikali, na nyingine zikajibiwa na Diwani wa Kata na Mbunge na kuwapa Wananchi miche bora ya migomba.


Katika ziara yake hiyo Mbunge aliambatana na Katibu wa CCM Wilaya ya Moshi Vijijini Ramadhan Mahanyu, Diwani wa Kata, Prospa Massawe, Diwani wa Viti Maalumu, Fabiola Massawe, Diwani Mstaafu wa Kata hiyo Deo Mushi, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (Halmashauri Kuu ya Kata), Wenyeviti na Watendaji wa Vijiji na Vitongoji, na wataalam toka idara mbalimbali za serikali.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI