Header Ads Widget

MBUNGE MBEYA VIJIJINI KUTOA SHILINGI LAKI 1 KWA WANAFUNZI WATAKAOFAULU KWA ALAMA A SHULENI.

Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza, ametembelea shule ya msingi Sayuma na kuhimiza wanafunzi kusoma kwa bidii akiahidi zawadi ya shilingi laki moja kwa wanafunzi wote watakaopata ufaulu wa alama A.


Njeza ametoa ahadi hiyo baada ya kutembelea kata ya Iwiji na kutembelea shule mbili katani humo na kuzungumza na wananchi.

Njeza amesikiliza kero za wananchi na kuahidi kuendelea kuzitatua kama ambavyo baadhi zimeendelea kutatuliwa ikiwemo ujenzi wa madaraja, usambazaji wa umeme na sasa kata yao imeahidiwa kujengwa kituo cha afya.


Njeza, ameahidi kuendelea kupigania kero zinazowakabili wananchi na wanafunzi mashuleni ili kuboresha maisha yao pamoja na mazingira ya utolewaji elimu ili kuongeza ufaulu shuleni.


Pamoja na motisha hiyo kwa watoto shuleni, pia Mbunge wa Mbeya vijijini anaendelea kuhimiza wazazi na walezi kuwekeza kwenye elimu na kuhakikisha wanatoa chakula cha mchana kwa watoto wao wawapo shuleni hatua ambayo itainua ufaulu katika shule mbalimbali jimboni Mbeya vijijini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI