Header Ads Widget

MBUNGE AWAANGUKIA WANANCHI KUNUSURU MRADI WA MAJI

 

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Asa Makanika akizungumza na mabalozi wa mashina, matawi na nyumba kumi  alipofanya ziara kwenye Kijiji cha Bitale Halmashauri ya wilaya Kigoma ambapo alifanya pia mkutano wa hadhara na wananchi. 

Wananchi wa kijiji cha Bitale wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Asa Makanika

(Picha na Fadhili Abdallah)

xxxxxxxxx

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini Asa Makanika amewaangukia wananchi wa Kijiji cha Bitale Halmashauri ya wilaya Kigoma kuruhusu upelekaji wa umeme kwenye kisima cha maji kitongoji cha Mlege maeneo ya Nyaruntengai li kuwezesha mradi huo kukamilika na kutoa huduma.

 

Makanika alisema hayo akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la madukani kwenye Kijiji hicho akieleza kuwa kukwama kutoa huduma kwa mradi huo kunaathiri idadi kubwa ya watu wenye mahitaji ya maji.

 

Mbunge huyo ameeleza kusikitishwa kwake na kukwama kwa mradi huo hasa kutokana na juhudi kubwa aliyofanya na kuongea na  Waziri wa maji, Jumaa Aweso ambaye aliagiza  kuchimbwa kwa visima viwili kwenye Kijiji hicho kunakotokana na changamoto kubwa ya maji iliyokuwepo kufuatia kukwama kutoa huduma kwa mradi wa Mkongoro.

Kufuatia hali hiyo Mbunge huyo  ameitaka TANESCO, RUWASA, kamati ya maji na uongozi wa serikali ya Kijiji kukaa na kujadiliana kuhusu changamoto hiyo na mwisho wa siku warudi kwa wananchi kuwaomba watoe maeneo yao kuweza kupitisha miundo mbinu ya umeme kuelekea kwenye kisima cha maji ili mradi uweze kutoa huduma.

 

 

Akielezea changamoto hiyo Balozi  kutoka kitongoji cha Mlege Kijiji cha Bitale, Yunusa Lubebanga akizungumza kwenye kikao cha ndani cha mabalozi alisema kuwa hawakuzuia mradi wa maji bali wamezuia kitendo cha watendaji wa shirika la umeme  (TANESCO) kukata miti yao ya michikichi ili kupitisha umeme bila kutoa maelezo yeyote kwao.

 

Kwa upande wake Mjumbe wa kamati ya mradi wa maji ya Kijiji iliyoteuliwa na Waziri wa maji Jumaa Aweso mwaka jana kusimamia mradi huo alisema kuwa kulikuwa na  uchimbaji wa visima viwili kwenye Kijiji cha Bitale alisema kuwa hadi sasa karibu michikichi 100  ya watu mbalimbali imekatwa licha ya kutolewa taarifa ya kupitishwa kwa umeme Kwenda kwenye kisima lakini  hakuna maelezo mengine kuhusu fidia ya mazao au nini kinapaswa kufanywa hivyo kusababisha mradi kusimama hadi sasa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI