Header Ads Widget

KAZI IMEANZA MBUNGE KABATI AWAPOKEA VIONGOZI WA CHADEMA

  

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Iringa (CCM), Dr. Ritta Kabati amepokea jumla ya wanachama watano wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa kata ya Ng'uruwe, Wilaya ya Kilolo.


Kabati amewakaribisha wanachama hao wa zamani wa CHADEMA wakiongozwa na aliyekua mwenyekiti wa BAWACHA wa kata hiyo, Sarah Mbwilo na Silvester Ngakonda wakati wa bonanza la Michezo lililoa ndaliwa na Umoja wa Vijana wa CCM kata ya Ng'uruwe na kufanyika katika viwanja vya Kihesa Mgagao.


Wakizungumza wakati wa kukabidhiwa kadi za Uanachama wa CCM, viongozi hao wa zamani wa CHADEMA wamesema wamefikia uamuzi wa kuhamia CCM kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh Dr. Samia Suluhu Hassan kuieltea Tanzania Maendeleo.


Kwa upande wake Mbunge Ritta Kabati ametoa wito kwa Watanzanja kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Tanzania inaendelea


Ameongeza kuwa maendeleo makubwa yanayofanywa na Rais Samia ni kwa ajili ya Watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI