Header Ads Widget

KAWAIDA ASISITIZA USHIRIKIANO WA VIONGOZI KATIKA UTENDAJI NDANI YA UVCCM



NA WILLIUM PAUL. 


Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Mohammed Ali Kawaida (MCC) amesisitiza  ushirikiano wa Viongozi wa Umoja wa Vijana wa CCM na Viongozi wa Serikali katika Utekelezaji wa Majukumu katika maeneo yao.


Kawaida ameyasema hayo akizungumza na Viongozi na Watendaji wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi Mikoa na Wilaya zote nchi nzima kwenye Ufungaji wa mafunzo ya Viongozi na Watendaji wa UVCCM yaliyofanyika Ihemi Mkoani Iringa. 



"Ndugu viongozi niwasihi sana twendeni tukafanye kazi kwa ushirikiano sisi kwa sisi na tupendane mpaka watu waliopo nje washangae, lakini pia tushirikiane na viongozi wa serikali katika Utekelezaji wa majukumu yetu kwenye maeneo yetu, tufuatilie Utekelezaji wa Ilani na kutangaza kazi nzuri zinazofanywa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika maeneo yenu" alisema Kawaida

Mwisho. 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI