Header Ads Widget

DK.MPANGO TUMEDHAMIRIA KUUFUNGUA MKOA KIGOMA KIUCHUMI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

MAKAMU wa Raisi Dk.Philip Mpango amesema kuwa serikali imedhamiria kuufungua mkoa kigoma kwa  miradi ya umeme  wa gridi ya Taifa na barabara za kiwango cha Lami kuwezesha kutekeleza mpango wa kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha uchumi na biashara kwa ajili ya fursa ya soko la nchi za ukanda wa maziwa makuu.

Makamu wa Raisi alissma hayo alipoanza ziara ya kiserikali ya siku saba mkoani Kigoma na kubainisha kuwa wakati wa mkoa Kigoma kufunguka kiuchumi ni sasa.


Akiwa katika kituo cha kupoza umeme eneo la Nguruka wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma Makamu huyo wa Raisi alisema kuwa  uwepo wa umeme wa gridi utawezesha kuvutia uwekezaji  katika viwanda vikubwa lakini pia viwanda vidogo ambapo bidhaa zitakazozaliswha zinazo fursa kubwa ya soko katika nchi za Burundi na Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.


Akiwa katika mradi wa barabara kilometa 51 kutoka Ilunde hadi Uvinza Makamu wa Raisi alisema kuwa serikali imedhamiria kuona sasa suala la barabara za vumbi kuunganisha mkoa Kigoma na mikoa mingine ifike mwisho ili barabara hizo ziweze kutekeleza mipango ya kiuchumi kwa miradi mikubwa na miradi ya wananchi wa kawaida.


Awali wa  Meneja wa mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme eno la Nguruka wilaya ya Uvinza, Mhandisi Sospeter Olalo kutoka TANESCO alisema kuwa hadi sasa ujenzi wa kituo hicho umefikia asilimia 95 na kazi ya umeme imeisha na sasa wanafanya majaribio mradi ukitarajia kukamilika August 30 mwaka huu.

 

Aidha alisema kwa sasa mradi wa njia ya kusafirisha umeme kilometa 304 kutoka Urambo Tabora hadi Kigoma inaendelea ambapo kwa upande wa kutoka Tabora hadi Urambo mkoani Tabora kilometa 105 imefikia asilimia 51 huku kipande cha kutoka Urambo mkoa Tabora Kidahwe mkoani Kigoma umbali wa 280 usanifu ndiyo unafanyika na mradi mzima umekamilika kwa asilimia 18.


Alipokea taarifa ya mradi wa barabara  Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Mohamed Besta akitoa taarifa kwa Makamu wa Raisi alisema kuwa barabara hiyo ya kilometa 51 imefikia aslimia 54 kwa sasa katika utekelezaji wake ambapo tayari kipande cha kilometa tisa kimeshakamilika kwa lami na kilometa tisa nyingine zinasubiri kuwekewa lami ambayo imekwama bandarini.


Sambamba na hilo Besta alisema kuwa mradi huo umekuwa ukisua sua kwa muda mrefu hali iliyofanya kumuondoa Mhandisi Mshauri Mkazi na kuweka mwingine hali iliyofanya mradi kuongeza kazi na sasa wanaamini radi utakamilika kwa wakati.

akitoa taarifa ya mkoa kwa Makamu wa Raisi kwenye ziara hiyo Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema kuwa mkoa unatekeleza miradi mbalimbali ambayo serikali imetoa kiasi cha shilingi trilioni 11.9  ambayo lengo ni kuufanya mkoa huo kuwa kitovu cha uchumi na biashara kwa fursa ya soko la nchi za maziwa makuu.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI