TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII
Na Fredrick Siwale -Matukio Daima APP - Mufindi.
KATIBU Siasa na Uenezi Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa , Ndg.Dickson Nadhani Lutevele,(Villa) ametupa jiwe gizani kwa kuwashambulia wale Wanaoisemea vibaya CCM
Ndg.Dickson Nathan Lutevele ( Villa) amesema hayo katika Mkutano wa hadhara uliofanyika Jimbo la Mafinga kwa Wananchi eneo la Kinyanambo "A"
Katika Mkutano huo pamoja na kuhudhuriwa na Wanachama wote wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Wananchi Viongozi wengine waliokuwepo ni Mwenyekiti wa CCM Wilayani ya Mufindi na Halmashauri ya Mji Mafinga pia waliokuwepo Wahe .Madiwa na Katibu Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa Ndg . Joseph Lyata.
Ndg.Villa alisema ni kumkosea sana Mhe.Rais DKT.Samia Suluhu Hassan Rais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Kwa kazi na miradi ya Maendeleo inayoonekana kutekelezeka.
" Kuna chama kimoja cha Kisiasa maarufu kwa jina la SACCOS kimekuwa kikiwalaghai Wananchi na kuwadanganya kuwa hakuna Maendeleo , hivi kweli kuona huoni na hata kusikia ! Hebu acheni Viongozi wetu waliopo Madarakani Waendelee kuchapa kazi kwa Vitendo na si vinginevyo.
Vyama vya Kisiasa Wilaya ya Mufindi vimetakiwa kushikiana kufanya Siasa ya Kiustaarabu na sio lugha za kuudhi kwa Wana CCM na Wananchi kwa ujumla.
Alisema CCM kwa sasa inawajulisha Wananchi utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2025 ikiwa na kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwa wingi kujiandikisha kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu 2024 na Uchaguzi Mkuu wa mwakani 2025.
Ndg.Villa aliwaambia Wananchi kuwa Maendeleo ya Viwanda Mufindi yamesaidia kuchangia pato la Taifa na kwa Vijana bila kubagua itikadi za Kisiasa wala Kidini na kuwataka Wananchi wawapuuze wanao beza mazuri ya Serikali ya CCM.
Upande wake Katibu wa Siasa na Uenezi Mkoa wa Iringa ,Ndg.Joseph Lyata umefika wakati wa Wana CCM kutembea kifua mbele na kufurahia mazuri yote yanayofanywa na kutekelezwa na Serikali ya CCM badala ya kubeza.
Ndg.Lyata alipongeza kasi ya Utendaji wa Viongozi wa CCM Wilaya ya Mufindi kwa speed waliyonayo kwa kuinadi Sera na Ilani ya CCM kwa Wananchi na kuisimamia vizuri Serikali bila uoga.
Aidha Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi Ndg.George Kavenuke Wapinzani waache Siasa za kitoto na badala yake wafanye Siasa za kushindana kwa hoja na sio vioja kwa Wananchi .
Alisema CCM Wilaya hadi kufikia sasa katika kipindi hicho cha amsha amsha ya " Tunazima zote tunawasha kijani" tayari mikutano 77 imefanyika na kazi inaendelea ya back to back hadi kieleweke.
Ndg.Kavenuke kwa niaba ya Wananchi wa Mufindi ametuma salaamu za Shukurani kwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan , kwa kuendelea kupanda Mufindi baada ya kumteua Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Mhe.Cosato Chumi kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kusema kuwa Mufindi itamchagua tena Dkt.Samia .
0 Comments