MOTO mkubwa umeibuka kwenye vibanda vya wafanyabiashara wadogo waliojenga kando ya kituo cha mabasi cha Msamvu ambapo vibanda zaidi ya kumi Kati ya 60 vilivyo eneo hilo vimeteketea.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamesema hili sio tukio la kwanza kutokea katika eneo hilo na inasadikiwa chanzo ni jiko la mkaa.
Hata hivyo Afisa Operesheni wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Mrakibu Msaidizi Daniel Myalla amesema bado waaendelea na uchunguzi kubaini chanzo cha moto huo ingawa katika hatua za awali wamefanikiwa kuudhibiti ili usilete madhara zaidi.
Mwisho
0 Comments