Header Ads Widget

VIJANA TUSIWE WABEBA MABEGI YA WAGOMBEA - JOKATE MWEGELO


TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

Katibu mkuu wa umoja wa chama cha mapinduzi Taifa (UVCCM) Jokate Mwegelo, amewataka vijana wa chama hicho kutokutumika vibaya kipindi hiki cha uchaguzi na wanasisa na kusahau nafasi zao ndani ya chama na kwenye jamii.


Amesema hayo wakati akizungumza na vijana wa mkoa wa Iringa, katika ofisi za chama cha mapinduzi mkoa, na kuwakumbusha vijana hao kutambua nafasi zao pamoja na malengo ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi.


Jokate amesema dhumuni la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM) ni kuwaanda vijana ili kuwa viongozi bora hapo baadae, hivyo kuendelea kutumika vibaya na wanasiasa hasa kipindi cha uchaguzi ama kuwa wakubeba mikoba ya wanasiasa wakongwe ni kushusha hadhi ya umoja huo.


"Vijana tusiwe wabeba mabegi ya watu wanaotaka kugombea kipindi hiki, tutatumika vibaya, tugombanishwa sisi wenyewe, tutatawanyika, tutasambaratika na kusahau kazi ya umoja wa chama cha mapinduzi. Alisema Jakate.


Aidha, Jokate amesema ofisi ya umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi taifa (UVCCM), hatakuwa tayari kupokea majungu, Fitina wala uchonganishi wa aina yoyote bali itatumika kuunganisha vijana na kuwasaidia kufikia ndoto zao bila kuangali vyama,dini, umri wala hali za vipata vyao.


Amesema ofisi hiyo itatumika kuwaanda vijana wa kitanzania kufikia ndoto zao kwa kuwaanda, kuwafundisha na kuwasimamia ili waweze kuwa viongozi bora baadae. 


"Ofisi ya katibu mkuu wa vijana itakuwa kiuunganishi cha vijana bila kuangalia vyama, dini wa hali zao za kipato kwani hayo ndiyo malengo ya chama cha mapinduzi CCM 


Pia Jakate amewasahauri vijana wa umoja huo kupendana,kusaidiana na kushikama ili kuweza kufikia malengo yao.


 
























Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI