Shirika la Madini la Taifa -STAMICO limetoa elimu kwa wachimbaji wadogo nchini kuachana na dhana potofu dhidi ya Watu wenye ualbino katika uchimbaji wao wa Madini kwa kuhusishanisha viungo vya wenye ualbino kwamba nikichocheo cha utajiri kwa wachimbaji.
Akitoa mada katika mkutano wa Wiki ya Madini mwaka 2024 MAIKO SALALI Mkurugenzi wa Taasisi ya Foundation for Disabilities Hope (FDH) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma ambapo Wachimbaji wadogo wamekuwa wakipata elimu za masuala mbalimbali kuhusu uchimbaji madini kupitia Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji nchini FEMATA.
Amesema Watu wenye ualbino ni binadamu kama binadamu wengine viungo vyao haviwezi kuleta utajiri hivyo wachimbaji waache dhana hizo potofu dhidi yao.
Alisema STAMICO inaendelea kutoa elimu ya kuondokana na dhana potofu katika makundi mbalimbali ya tasinia ilikuondoa dhana potofu zinazopelekea hatari kwa walemavu na Watu wenye ualbino nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa SATAMICO Dr. Venance Mwasse Meena amesema wameamua kuwasaidi Watu Wenye huitaji maalum Kwa kuwapa kontena Ili waweze kuuza mkaa mbadala ikiwa ni pamoja na kuwawezesha uchimbaji wa Madini.
Amesema kundi la walemavu wa usikivu wamewawezesha Mgodi wa Wachimbaji wa Madini ambao wapo kwenye hatua za mwisho kuanza kupata Madini.
0 Comments