Header Ads Widget

MVUA CHANZO CHA KUCHELEWA KUMALIZIKA KWA MIRADI YA REA LINDI

 


NA MWANDISHI WETU


Lindi.Licha ya baadhi ya wakandarasi kufanya kazi kwa kasi ndogo lakini asilimia kubwa ya vijiji mkoani Lindi vimefikiwa na huduma ya umeme.


 Mkuu wa wilaya ya Lindi Shaibu Ndemanga akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa amesema licha ya kuwapo kasi ndogo ya utekelezwajibwa miradi lakini hali inaridhisha sana.


"Zipo changamoto ambazo tumeshauriana ikiwepo kasi ndogo ya utekelezaji wa miradi ambayo sio mzuri tumekubaliana na mwenyekiti wa bodi na wajumbe wake kuwa watapita kuangalia miradi yote na miradi hii ilitakiwa imalizike mwisho wa mwezi June lakini kuna kila dalili isimalizike"


Kikubwa walichokuja kufanya ni kuangalia  miradi tunayo itekeleza yakusambaza umeme mkoa wa Lindi.Tuna vijiji takribani 524  na vyote vilipaswa kufikiwa na umeme wa REA na 75% ya vijiji hivyo vimefikiwa n umeme" amesema Ndemanga.


Ndemanga aliendelea kusema kwa wilaya ya Lindi kasi ni mzuri hadi kufika mwezi machi kati ya vijiji 140 vilibakia 23 lakini vijijivilivyobakia hadi sasa ni kama 10  lakini bado kuna kazi ya ziada  kuna jitihada zinazotakiwa kufanyika ili kuona  miradi inakamilika kwa haraka iwezekanavyo.


"Tumefikisha umeme kwenye vijiji lakini kwa sasa tunakazi yakupeleka umeme kwenye vitongoji  katika kila jimbo.Kufikisha umeme kwenye Vijiji haimanishi tumepeleka kwenye kila kitongoji pia tumejadili kuhusu kupeleka umeme kwenye sehemu maalumu kama Vituo vya Afya,Vyazo vya maji mradi umeanza lakini watajadili kuona wanatekeleza kwa kasi"amesema Ndemanga. 


Mwenyekiti wa  bodi ya REA Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu amesema  mvua  nyingi zilizonyesha ni moja ya changamoto iliyo sababisha kuchelewa kumalizika kwa miradi kutokana na kuharibika kwa miundombinu ya barabara yakufika huko vijijini.



"Hali iliyo jitokeza ya majanga ya mvua iliyo haribu miundombinu ya barabara  inayowezesha kufika Vijijini imekuwa ni changamoto kukamilisha kwa wakati miradi.Tanesco na Rea ni ndugu wapo  kwenye wizara moja wanategemeana na ikikamilika wanakabidhiwa Tanesco hivyo tunashirikiano mkubwa sana"amesema Kingu.


Pia aliongeza kwa kusema meneja wa wilaya au mkoa Tanesco anakuwapo kuhakikisha viwango vya mradi unaotekelezwa na mkandarasi.Miradi inayo tekelezwa inagarimu takribani sh 96 bilioni.


Naye Meneja wa shirika la umeme mkoa wa Lindi (Tanesco)Athumani Jumbe amesema vijiji  515 tayari miradi imeshakamilika  bado vijiji 9 tu ambavyo  bado havijakamilika.


"Mkoa wa Lindi tuna vijiji 524 hadi leo vijiji 515 vimeshafikiwa na umeme bado 9 wilaya ya Kilwa 7 na wilaya ya Lindi mjini vijiji 2 Nachingwea na Ruangwa vimeshakamilika.Bado tupo kwenye hatua ya kuunga wateja tunamiradi ya ndani ya Tanesco na kuna ya REA".


"REA inamiradi ya aina nne mradi wa uviko,Machimbo ya madini na kilimo cha umwagiliaji,Rea awamu ya 3 mzunguko wa pili unaomalizia zoezi la upelekaji wa umeme awamu ya pili na kuna mradi wakupeleka umeme kwenye vitongoji na mradi umesha anza tutapeleka kwenye vitongoji 288 na utakapo malizika eneo kubwa litakuwa litakuwa limefikiwa na umeme"amesema Jumbe Meneja wa Tanesco mkoa wa Lindi.


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI