Na Hamida Ramadhan matukio Daima app Dodoma
MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa kushirikiana na mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) wameingia mkataba wa mashirikiano ya kupatia Huduma za Afya wanacha wa ZHSF Tanzania Bara lengo likiwa ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za afya za uhakika na endelevu kwa wananchi na wakazi wote wa Zanzibar
bila kuwa na kikwazo cha fedha pale wanapozihitaji .
Makubaliano hayo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa rasilimali fedha za kutosha katika kugharamia huduma za afya.
Akiongea katika kikao hicho cha makabidhiano kilichofanyika leo Juni 28 jijini Dodoma Bernard Konga Mkurugenzi Mkuu wa NHIF amesema,
Mwaka 2023 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ilianzisha Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHSF) kwa kuhakikisha kuwa ZHSF inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar Na. 1/2023.
" Kutambua uzoefu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), katika uendeshaji wa mfumo wa bima ya afya nchini, Julai Mosi, 2024 ZHSF itaanza rasmi majukumu yake kwa kuhudumia wanachama na wategemezi wake kupitia Vituo vya kutolea huduma vilivyosajiliwa na NHIF Tanzania Bara, " Amesema
Na kuongeza "Katika kufanikisha huduma kwa wanachama hao, NHIF na ZHSF zimesaini mkataba wa makubaliano wa mashirikiano katika utoaji wa huduma kwa
wanachama wake, " Amesema Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Konga
Amesema hatua hii inatokana na uzoefu, wigo mpana wa vituo vya
kutolea huduma vilivyosajiliwa na NHIF nchi nzima.
Ameeleza Maandalizi yaliyofanywa na NHIF kwa upande wa NHIF, hatua mbalimbali za maandalizi na utayari wa
kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa mashirikiano zimefanyika ili
kuhakikisha wanachama hao wanapata huduma bila ya changamoto yoyote.
Aidha amesema Ofisi zote za NHIF zilizoko katika Mikoa yote ziko tayari na
zimejipanga kutoa huduma na kutoa msaada utakapohitajika, Mifumo ya utambuzi imeimarishwa zaidi ili kurahisisha utambuzi wa wanachama wanapofika katika vituo vya kutolea
huduma, Kufanya malipo kwa watoa huduma kwa wakati pindi
wanachama hawa watakapopata huduma za matibabu katika
vituo husika, Kuandaa Ofisi kwa aiili watumishi wa ZHSF watakaokuwa
wanahudumia wanachama kwa upande wa Tanzania Bara.
Amesema Utaratibu utakaotumika kwa wanachama wa ZHSF kupata huduma za matibabu, Wanachama wa ZHSF watapata huduma kwa kuzingatia sheria, kanuni na miongozo ya tiba nchini kama inayotumika kwa wanachama wa NHIF. Taratibu hizo ni pamoja naWanachama na wategemezi wa ZHSF watatumia kadi ya uanachama ya ZHSF badala ya kadi ya NHIF.
Vituo vitatumia Mifumo ya utambuzi inayotumiwa na NHIF
katika kuhakiki uhalali wa wanufaika;
Kutumia mfumo wa rufaa katika kupata huduma ambapo
mwanachama anaweza kuanzia ngazi ya hospitali ya wilaya ama ngazi ya
chini kupata huduma husika.
Ushughulikiaji wa Changamoto za Kihuduma Katika kuhakikisha wanachama wanapata huduma wanazohitaji, ZHSF na NHIF zimejipanga kwa kuweka Maofisa Maalum kutoka ZHSF ambao watakuwa katika Ofisi za NHIF kwa ajili ya kushughulia changamoto zinazojitokeza hususan za kihuduma.
Aidha kwa sasa Hospitali nyingi za NHIF zinayo madawati maalum ya Watum1shi wake ambao moja ya majukumu yao ni kutoa usaidizi kwa wanachama wanaokwama ama kukutana na changamoto katika kupata huduma za matibabu.
Mfuko unawahakikishia wanachama wake upatikanaji wa huduma bora Za
matibabu katika vituo vyote wa kutolea huduma vilivyosajiliwa na MYuko.
Yasin Juma Mkurugenzi Mkuu wa mfumo wa wa Huduma za Afya Zanzibar ZHSF amesema Kuanzia mwezi wa Julai, 2024 watumishi ambao walikuwepo NHIF kutoka sekta ya umma watarudi rasmi ZHSF na wafanyakazi wote waliopo sekta binafsi wataanza kupata huduma ZHSF kuanzia tarehe 1 Septemba, 2024. Vilevile ZHSF itafungua ofisi Tanzania Bara ili kuratibu kwa ukaribu maswala yetu.
Amesema Mwezi wa Machi, 2024 ZHSF ilianza usajili wa sekta Binafsi na huku tukiandaa mikakati ya kuelekea katika usajili wa sekta isiyo rasmi na makundi mengine yasiyokuwa na uwezo kama ilivyoelekezwa katika Kifungu cha 2 cha Sheria ya Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar Nam.1 ya 2023.
"Katika kipindi cha mpito cha kuwafikia wanachama wetu walioko Tanzania Bara, tulishirikiana na wenzetu wa NHIF ili kuweka utaratibu wa muda wa kuwawezesha wanachama hao kupata huduma za afya, ambapo ZHSF ilikua ikilipa michango ya wanachama hao NHIF," Amesema
Na kuongeza "Vilevile, ZHSF na NHIF zilikua zikishirikiana kwa wanachama wote ambao kabla ya kuanzishwa kwa ZHSF walikua ni wanachama wa NHIF ambapo hadi sasa NHIF inaendelea kuwapatia huduma wanachama hao kwa kutumia kadi za NHIF, "
Hata hivyo amebainisha kuwa Kwa mujibu wa kifungu cha 27 cha Sheria Nam.1 ya 2023, Mfuko umepewa uwezo wa kuwafikishia wanachama wake huduma za afya nje ya Zanzibar, ambapo kwa kuanzia ZHSF imeanza kuwafikia wanachama wake walioko Tanzania Bara.
"Tukio la leo linaakisi utekelezaji wa masharti ya Sheria hiyo Hivyo basi, mafanikio haya ya kufikia makubaliano na wenzetu wa NHIF ni ya kujivunia kwani yatawawezesha wanachama wetu kupata huduma za afya wakiwa Tanzania Bara kwa kutumia kadi za ZHSF, " Amesema
0 Comments