Header Ads Widget

MALISA AACHIWA KWA DHAMANA AENDE HOSPITALI KULAZWA

 


Jeshi la Polisi limemuachia kwa dhamana Mchambuzi wa Masuala ya Kijamii na Kisiasa, Godlisten Malisa ambaye alikuwa anashikiliwa kwa mahojiano ya tuhuma kadhaa kuhusu taarifa alizoziandika kwenye Mitandao ya Kijamii


Mmoja wa Mawakili wanaomsimamia, Wakili Hekima Mwasipu amesema "Malisa amehojiwa mara mbili, tulikuwa tunasubiri ahojiwe mara ya tatu, ameachiwa kwa dhamana na kusaini bondi ya Tsh. Milioni 10, ilikuwa Saa Saba Usiku kwa maelekezo kuwa leo (Juni 8, 2024) Saa Tatu Asubuhi nimpeleke kwa ajili ya mahojiano ya mara ya tatu."


Ameongeza "Tulipotoka tukampeleka Hospitali ya KCMC kwa kuwa Afya yake haikuwa vizuri, ana homa, kifua kinamsumbua na mwili uliishiwa nguvu."

MALISA ALAZWA :


Baada ya Mwanaharakati na Mkurugenzi wa GH Foundation, Godlisten Malisa kukaa mahabusu kwa zaidi ya saa 24, katika kituo cha polisi Moshi kati, Mkoani Kilimanjaro, Mwanasheria wake, Hekima Mwasipu amesema mteja wake huyo aliugua akiwa mahabusu na baada ya kupewa dhamana usiku wa kuamkia leo Juni 8 alipelekwa hospitali ya KCMC kwa matibabu.


Mwasipu amesema mteja wake huyo alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kichwa, kifua, kizunguzungu na tumbo na kwamba afya yake kwa sasa imeimarika.


Malisa alikamatwa Juni 6, 2024 muda mfupi baada ya kesi inayomkabili yeye na Meya wa zamani wa ubungo, Boniface Jacob kuahirishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam.


Akizungumza na Mwananchi digital leo asubuhi, Juni 8, Mwanasheria wake, Hekima Mwasipu amesema, Malisa baada ya kukaa kituo cha polisi kati Moshi, Malisa aliugua gafla na alipopata dhamana aliwahishwa KCMC kwa matibabu.


"Tulipopata dhamana usiku wa saa 6 kituo cha polisi Moshi kati, tulimpeleka hospitali ya KCMC moja kwa moja kwa sababu alikuwa akilalamika maumivu ya kichwa, kifua, kizunguzungu na tumbo,"


"Alipatiwa matibabu na tulirudi saa 10 alfajiri, kwa sasa anaendelea vizuri," amesema wakili wake Mwasipu.


Endelea kufuatilia Matukio Daima media na mitandao yetu TIKTOK,BLOG , YOUTUBE N.K 

TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI