Header Ads Widget

KITUO CHA AFYA URU KUSINI KUPATA VIFAA TIBA...

 


NA WILLIUM PAUL. 

WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu amemuhakikisha Mbunge wa Jimbo la Moshi vijijini, Prof. Patrick Ndakidemi kuwa serikali itapeleka vifaa tiba vya kisasa katika kituo cha Afya Uru kusini ambacho kinatarajia kuanza kutoa huduma muda sio mrefu. 

Hatua hiyo ni neema kubwa kwa wananchi wa kata ya Uru kusini na maeneo jirani ambayo itawapelekea kutotembea umbali mrefu kufuata huduma ya Afya. 

Hayo yamejiri baada ya Mbunge Prof. Patrick Ndakidemi kuuliza swali la nyongeza je serikali inampango gani wa kununua vifaa tiba katika kituo cha Afya Uru kusini ambacho ni kipya na kinatarajiwa kuanza kutoa huduma karibuni. 

"Waziri Ummy umenisaidia sana kwenye Jimbo langu kunipatia vifaa tiba katika vituo vya Afya Umbwe na Uru kiasini je serikali inampango gani wa kutusaidia vifaa tiba katika kituo cha Afya Uru kusini ambacho ni kipya na kinatarajiwa kutoa huduma karibuni" Alihoji Prof. Ndakidemi. 

Akijibu swali hilo, Waziri Ummy alisema kuwa, kupitia bajeti ya fedha ya Ofisi ya Rais na Serikali za mitaa Tamisemi na Wizara ya Afya wametenga fedha kwa ajili ya kununua vifaa tiba na vitasambazwa katika vituo vyote vya Afya. 

Alisema kuwa, na hii ni kazi nzuri ambayo Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameifanya katika nchi kuhakikisha vifaa tiba vya kisasa vinapatikana katika ngazi ya zahanati na ngazi ya vituo vya Afya. 

Waziri huyo Ali kuhakikisha Mbunge Ndakidemi wananchi wa Uru kusini watapata vifaa tiba kabla ya uchaguzi mkuu mwakani.. . 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI