Header Ads Widget

KASSIM MAJALIWA AZINDUA MFUMO WA SMARTWASOMI UTAKAWOWASAIDIA WANAFUNZI.

 


NA AMINA SAIDI,TANGA.

Serikali kwa kupitia wizara Elimu ikishirikiana unicef na Airtel Tanzania imeandaa majukwaa mawili makuu yakidijitali ambayo yatasaidia kuimarisha matumizi ya tehama katika kufundisha na ujifunzaji.


Aidha majukwaa hayo ni maktaba ya mtandao  pamoja na mfumo wa ufundishaji na ujifunzaji kwa walimu ambào unatumika kwa walimu mafunzo endelevu kazini  unaojulikana kwa jina la Mewaka .

 

Hayo aliyasema mkurugunzi  mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzinia (TET)Dkt.Annet Komba wakati wa uzinduzi wa mfumo wa Airtel smatwasomi inayosimiwa na kampuni ya Artel Tanzani kwa kushirikiana na Unicef  wakiwa katika maonyesho ya  kitaifa ya Sayansi Teknolojia na ubunifu yaliyofanyika katika viwanja vya shule yaPopatlal jijini Tanga.


Aliongeza kusema kuwa majukwaa hayo yamepatiwa maudhui mbalimbali yakiwemo vitabu vya kiada,vitabu  vya kiada mtaala ulioboreshwa na mtaala ambao tutaendeleea kuukamilisha.


Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji  wa Airtel Tanzania Dinesh Bahsingb alisema kuwa lengo kuu ni kuimarisha matumizi ya tehama katika ufundishaji na ujifunzaji hususani kwa vijana wanaosoma mashulenj na vyuoni kwani matumizi ya internet yakuwa rahisi.


Waziri mkuu kassim Majaliwa  aliwapongeza kampuni ya Aitel kwa kuja na mradi  huo wa smatwasomi kutokana na manufaa makubwa katika jamii.


Katika hatua nyingine mkuu alizindua mfumo wa  smatwasomi inayosimamiwa na kampuni ya Airtel Tanzania  kwa kushirikiana na  Unicef itakayosaidia wanafunzi kujinza kwa njia ya tehama.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI