Header Ads Widget

CHADEMA MBEYA YADAI RAIS SAMIA NI MWEPESI KUMSHINDA UCHAGUZI UJAO.

NA JOSEA SINKALA, MBEYA.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mbeya Masaga Kaloli amesema uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu CHADEMA itahakikisha inashinda kwani Chama Cha Mapinduzi kumpitisha Rais Samia Suluhu Hassan ni kuipa CHADEMA ushindi.


Masaga, amewataka wananchi mkoani Mbeya kuachana na Chama Cha Mapinduzi CCM kwa madai kuwa kimeshindwa kuwaletea wananchi maendeleo.


Masaga ameeleza hayo wakati akihutubia kwenye mkutano wa hadhara wa chama hicho (CHADEMA) ambao umefanyika katika kata ya Ndanto jimbo la Rungwe mkoani Mbeya ambapo Chama cha Mapinduzi kimeshindwa kuwaletea maendeleo wananchi wake pamoja na kuzuia uhuru wa wananchi kuwahoji viongozi wao hivyo kueleza umuhimu wa kupatikana kwa katiba mpya.


Masaga amenukuliwa akisema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni mwepesi hivyo CHADEMA inakwenda kushinda uchaguzi mkuu ujao pamoja na uchaguzi wa Serikali za mitaa baadaye mwaka huu.


Mwenyekiti wa CHADEMA jimbo la Mbeya vijijini Getruda Japhet Lengesela, ametumia mkutano huo kuwataka wenye nia na uwezo hususani wanawake kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali kwenye uchaguzi ujao ili CHADEMA kuleta mapinduzi ikiwa itaaminiwa na wananchi.


Naye mwenyekiti wa baraza la wazee la Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA (BAZECHA) mkoa wa Mbeya David John Mwambigija, ameeleza kuwa pamoja na CCM kuwa madarakani kwa zaidi ya miaka sitini bado kuna maeneo hayana huduma ya maji safi na salama.


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Mbeya kinaendelea na mikutano yake ili kuwafikia wanachama na wananchi kwa ujumla kikieleza kuwa madhumuni yao ni kuhakikisha wanatoa elimu ya uraia kwa wananchi na kuwaomba wawachague CHADEMA kwenye chaguzi zijazo ili kuwaletea maendeleo ambayo yamekuwa yakihubiriwa na CCM muda mrefu bila mafanikio ya wazi.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI