CHAMA Cha Mapinduzi (CCM ) mkoa wa Iringa kimechangia kiasi Cha Tsh milioni 9 kuunga mkono ujenzi wa chumba Cha wagonjwa Mahututi (ICU) Hospitali ya Ipamba wilaya ya Iringa.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa Comrade Daud Yassin amekabidhi mchango huo leo Jumatano Juni 5, 2024 kufuatia ziara ya pamoja baina yake na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (MNEC) Salim Abri Asas baada ya kutembelea hospitali hiyo kwa lengo la kuangalia maendeleo ya ujenzi wa ICU.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mchango huo wa CCM, Yassin alisema CCM Mkoa wa Iringa wameamua kuwa karibu na jamii pamoja na taasisi zote zinazotoa huduma halali kwa wananchi zikiwemo za kidini.
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Iringa Daud Yassin aliyeambatana na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa (NEC) Salim Abri Asas na viongozi wengine wamekabidhi mchango huo ikiwa ni uungaji mkono jitihada za Hospital hiyo pia jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika uboreshaji wa Sekta ya Afya nchini .
Kwa upande wake, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Salim Abri Asas ametoa pongezi kwa madaktari na wauguzi wa hospitali hiyo Ipamba -Tosamaganga kutokana na huduma nzuri wanazotoa kwa wagongwa wakati wote.
Ili kuunga mkono ujenzi wa ICU Hospitali ya Tosamaganga (Ipamba ) changia kupitia Lipa Tigo
6854055 au CRDB 0150 243298100
0 Comments