Header Ads Widget

BREAKING NEWS:GARI LA TANESCO LAPATA AJALI

 

Majeruhi wa ajali ya gari la Tanesco wakiwa eneo la Tukio 





Habari zilizotufikia hivi Punde kutoka Mafinga wilayani Mufindi mkoani Iringa zinadai watu kadhaa wanahofiwa kupoteza maisha baada ya lori la kampuni ya Tanesco kupinduka wakati likijaribu kumkwenda mwendesha Baiskeli.


Ajali hiyo imetokea eneo la majinja Changarawe Mjini Mafinga katika barabara kuu ya Iringa -Mbeya kwa Lori Hilo lililobeba wafanyakazi wa TANESCO kupinduka.


Mashuhuda waliozungumza na Matukio Daima media wamesema hadi sasa badi idadi kamili ya waliofariki haijajukana  japo miili zaidi ya mmoja ilikuwa imelazwa chini.


Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda Selekwa amethibitisha kutokea ajali hiyo na kuwa imetokea saa 12:45 jioni na kuwa hadi sasa vifo ni watu wawili na wengine wamejeruhiwa japo taarifa kamili ataitoa baada ya kupata habari kamili .

Matukio Daima media tunaendelea kumtafuta kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa ili kupata habari kamili na tutakujuza hapa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI