MSIMAMIZI wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kwahani Unguja Safia Iddi Mohammed amemtangaza mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Khamis Yussuf maaruf Pele kuwa Mbunge wa Jimbo hilo.
Safia amemtangaza Pele kushinda nafasi hiyo leo Jumamosi, Juni 08,2024 usiku katika ukumbi wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi Lumumba mkoa wa mjini Magharib Unguja.
Amesema kuwa mshindi huyo amepara kura 7092 akifuatiwa na mgombea wa chama ADC kura 83 na kufuatiwa na Ada Tadea kura49 na Cuf kura 79.
" Chama CCK kura 21, Demokrasia makini kura 14 , Dp kura 7,NRA kura 8 na NLD kura 5, SAU kura 7, UDP kura 1," amesema.
Uchaguzi huo umejuisha 14 vya siasa, kufuatia kifo cha aliekuwa mbunge wa jimbo hilo Yahaya Ahmada kilichotokea Aprili mwaka huu.
Awali Msimamizi huyo amesema kuwa, Jimbo la kwahani lina idadi ya wapiga kura 11936,kura halali. 7522 na kura zilizoharibika 139.
"Kwa mamlaka nilionayo napenda kumtangaza ndugu Khamis Yusuf Mussa kuwa mbunge wa jimbo la kwahani Unguja kwa akiongoza idadi ya kura 7092," amesema.
Kwa upande wake mshindi wa Uchaguzi huo Mdogo Khamis Yussuf Mussa Pele amewashukuru Wanachama wa chama cha Mapinduzi kwa kuwa na imani kwa kumchagua kuwa Mbunge wa jimbo hilo.
Mapema kuu wa Chama cha Demokrasia Makini Ameir Hassan Ameir ameeleza kuridhshwa na uendeshaji wa zoezi la kupiga kura katika uchamguzi mdogo wa Jimbo la Kwahani Unguja.
Ameir amesema zoezi hilo limeendeshwa kwa amani na utulivu huku Wananchi wakiendelea kutumia haki yao ya kidemokrasia ya kuchagua mbunge wa jimbo hilo.
Amesema chama cha Demokrasia makini kimejipanga kuchukua ubunge katika jimbo hilo na kuhakikisha wanawaletea Maendeleo wananchi wa jimbo hilo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa chama cha UPDP Hamad Ibrahim ameipongeza Tume huru ya uchaguzi kwa kuendesha zoezi hilo kwa uhuru na haki.
0 Comments