Header Ads Widget

WEZARA YA ELIMU KUTEKELEZA VIPAUMBELE VITANO MWAKA WA FEDHA 2024/25


 


Na Hamida Ramadhan Matukio  App Dodoma

WIZARA ya Elimu, Sayansi, na Teknolojia, amesema vipaumbe vya Wizara hiyo katika mwaka wa fedha 2024/25  Wizara imepanga kutekeleza vipaumbele vitano vyenye lengo la kuongeza ubora wa elimu kwa kuwezesha vijana wa Kitanzania kupata maarifa, ujuzi, kujiamini, kujiajiri na kuajirika. 

Akisoma Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Waziri Prof.Adolf Mkenda Vilevile, vipaumbele vyenye kujielekeza katika kutegemeza tafiti, sayansi, teknolojia na ubunifu katika agenda ya maendeleo ya nchi.

Ametaja vipaumbele vya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/25 kuwa ni kuendelea na utekelezaji wa sera na mitaala, mapitio ya sheria na kuandaa miongozo ya utoaji elimu na mafunzo nchini.

Kipaumbele kingine ni kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (amali na amali sanifu),

Pia amesema kipaumbele kingine ni kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya msingi, sekondari na ualimu,kuongeza fursa na kuimarisha ubora wa elimu ya juu na kuendeleza tafiti, matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

Aidha Waziri Mkenda imeliomba Bunge kuidhinishiwa jumla ya Tsh.Trillioni Moja, Bilioni Mia tisa Sitini na Nane, Milioni mia mbili kumi na nane na elfu Mia tano na thelathini na nne (1,968,218,534,000.00.)ya Makadirio ya Mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2024/ 2025.

Amesema ili kuwezesha utekelezaji wa malengo kwa mwaka wa fedha 2024/25, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (Fungu 46) inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 1,965,330,380,000.00 kwa mchanganuo ufuatao

“Mheshimiwa Spika Shilingi 637,287,706,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara ambapo Shilingi 585,225,031,000.00 ni kwa ajili ya Mishahara na Shilingi 52,062,675,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo na Shilingi 1,328,042,674,000.00 zinaombwa kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo ambapo Shilingi 1,033,393,669,000.00 ni fedha za ndani na Shilingi 294,649,005,000.00 fedha kutoka kwa Washirika wa Maendeleo.

"Mheshimiwa Spika, Wizara kupitia Tume ya Taifa ya UNESCO (Fungu 18) inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 2,882,154,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ambapo Mishahara ni Shilingi 1,319,040,000.00 na Matumizi Mengineyo ni Shilingi 1,563,114,000.00.

"Mheshimiwa Spika, kwa heshima kubwa naomba sasa Bunge lako tukufu likubali kupokea, kujadili na kupitisha Makadirio ya Bajeti ya Wizara (Fungu 46 na Fungu 18) yenye jumla ya Shilingi 1,968,212,534,000.00,"amesema Prof. Mkenda

Vilevile Serikali imesema katika kuboresha miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika ngazi ya elimu ya msingi, sekondari na ualimu,itawezesha ujenzi wa shule za sekondari za kata 226, nyumba za walimu 184 wa sekondari na ununuzi wa vifaa vya maabara.

Ambapo amesema serikali itawezesha ujenzi wa madarasa 2,018 (msingi 1,221 na sekondari 797),mabweni 114 kwa shule za sekondari,nyumba za walimu 658 (msingi 567 na sekondari 81) matundu ya vyoo 2,848 (msingi 1,514 na sekondari 884), maabara 10 na vituo vya walimu (TRCs) 300 kwa lengo la kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji. 

Aidha,amesema itakamilisha ujenzi vyumba vya madarasa 111 katika shule za msingi 37, matundu ya vyoo, maabara, nyumba za walimu na mabweni katika shule za sekondari 50 na itaweka nishati safi ya kupikia ili kuendelea kuhifadhi na kuimarisha mazingira katika vyuo vya ualimu 11 (Nachingwea, Katoke, Kleruu, Tabora, Dakawa, Patandi, Mpwapwa, Sumbawanga, Mhonda, Kasulu na Monduli). 

Vilevile, itanunua samani kwa ajili ya Chuo cha Ualimu Sumbawanga, Mhonda, Dakawa na Ngorongoro.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI