Header Ads Widget

WATANO WAJERUHIWA NA MAMBA DAR, TAWA WATAADHARISHA WANANCHI

 





TAZAMA VIDEO BOFYA LINK HII

Na Scolastica Msewa, Kigamboni 

Mhifadhi wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania – TAWA - kanda maalum ya Dar es salaam, ZAWADI MALUNDA amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam kuchukua taadhali ya mamba na kiboko kutokana na wanyama hao kuletwa na maji yaliyotokana na mafuriko ya maji kutoka kwenye mito kuelekea baharini wanyama hao wakali wanaweza kuwa wamebaki katika mito na madimbwi mitaani na kwenye makazi ya watu na kusababisha athari kwa jamii.


Amesema hayo kwenye viwanja vya kusanyiko la Mwenge wa Uhuru wa mwaka 2024 wilaya ya Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo TAWA walikuwa wakitoa elimu kwa wananchi kuhusu uwepo wa wanyama wakali hao ambao wamesababishwa na uharibifu wa mazingira.


Amesema wanyama hao wakali husombwa na maji ya mito inapofurika kuelekea baharini kupitia mito, vijito na maji yaliyotuams majirani na makazi ya watu na kuweza kusababisha athari kwa jamii.


Aidha amewataka wananchi kutoendesha shughuli zao ndani ya madimbwi, mito, mabwawa bila tafadhali ikiwa ni pamoja na kulima katika umbali wa zaidi ya mita 60 kutoka kwenye vyanzo vya maji.


Kwa upande wake Sanjo Mafuru Mhifadhi wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyama pori Tanzania – TAWA - kanda maalum ya Dar es salaam ameonya tabia ya baadhi ya wananchi wanaoharibu kingo za mto, vyanzo vya maji, wanaofanya shughuli za uvuvi haramu wa kutumia sumu pamoja na shughuli za kilimo zimetajwa kuwa chanzo cha mamba na kiboko ambao hulazimika kuyahama makazi yao ya asili na kukimbilia kwenye maficho yaliyo jirani na makazi ya watu na hivyo kuhatarisha maisha ya binaadamu.


Amesema mahali penye vitendo vya uharibifu wa mazingira panakuwa na kujitokeza kwa vichocheo vya mabadiliko ya tabia nchi ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa mvua nyingi zinazosababisha mafuriko au kiangazi kikavu kinachosababisha wanyama pili kutoka eneo moja kwenda jingine hata kwenye makazi ya watu hasa makazi yaliyokaribu na vyanzo vya maji.


Sanjo ameitaka jamii wajiepushe na uharibifu wa mazingira ambao umekua ukiathiri kwa kiasi kikubwa usalama wa wanyama ambao pia ni vivutio.


Naye Luciana Bashaija Afisa wanyama Poli katika Halmshauri ya wilaya ya Kigamboni amesema Watu watano wameripotiwa kujeruhiwa na mamba katika wilaya hiyo na kuwataka wananchi kuchukua tafadhali hasa wanapopita kwenye madimbwi ya maji, mito.


Amesema wanaendelea kutoa elimu kwa jamii kuchukua tafadhali kuhusu kuwepo kwa wanyama hao wakali kwenye makazi ya watu walioletwa maji ya mafuriko ya mito na vijito.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI