Header Ads Widget

WAJASILIAMALI WATAKIWA KUZINGATIA MATUMIZI SALAMA YA KEMIKALI.

 


WAJASILIAMALI wadogo na kati wanaozalisha bidhaa zinazotumia kemikali wametakiwa kutumia kemikali hizo kwa usalama ili zisisababishe madhara kwao na kwa watumiaji wengine.


Ushauri huo umetolewa mjini Iringa na Meneja wa Mamlaka ya Maabara ya mkemia Mkuu wa Serikali kanda ya kati Dodoma Bw Gerald Meliyo Mollel  wakati wa mafunzo kuhusu utumiaji na uhifadhi sahihi wa Kemikali kwa wajasiriamali wadogo na wa Kati wa mkoa wa Iringa wanaozalisha bidhaa zinazotumia kemikali.



Akasema kwa siku za hivi karibuni wameibuka wajasiliamali wengi wanaozalisha bidhaa zinazotumia Kemikali ikiwemo sabuni ya maji na Batiki lakini hawana elimu sahihi na ya kutosha juu ya madhara yanayoweza kuwapata iwapo hawatachukua tahadhari.


"Kemikali zina madhara kiafya pale usipo fuata taratibu kwa kuvaa vifaa Tiba kama vile kofia ngumu, glavu, barakoa ili kujilinda pale wanapo guswa na Kemikali hizo ambazo huathiri ngozi na kusababisha kansa, upofu na kuharibu mazingira zikitupwa ardhini bila utaratibu" Amesema


Akasema mbali na kutokujua matumizi salama ya Kemikali hizo wajasiliamali wengi hawakuwa na Elimu sahihi ya kusafirisha na kutunza Kemikali hizo.


"Wajasiliamali wengi wanatabia ya kuhifadhi Kemikali ndani ya Nyumba pale wanapo maliza kuzitumia jambo hili ni hatari kwani Kemikali nyingi zinatabia ya kulipuka, kuunguza hivyo ni hatari na haipaswi kuhifadhi ndani ya Nyumba" Alisisitiza


Nao wajasiliamali waliofikiwa na mafunzo hayo wameshukuru Serikali kupitia mamlaka ya Maabara ya mkemia Mkuu wa Serikali kuwafikishia elimu hiyo bure na kuwagusa wajasiliamali zaidi 80.



"Jamii yetu haiepuki matumizi ya Kemikali kwani bidhaa nyingi tunazotumia zinazalishwa na Kemikali hivyo mafunzo haya yamekuja wakati muafaka na yametuachia somo na Elimu kwa wajasiliamali kwenda kuzalisha bidhaa bora huku wakijua namna ya kujilinda usalama wao na wa wengine." Alisema mmoja wa wajasiriamali Omary Sanyagi.


Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI