Header Ads Widget

WAHITIMU WA MAFUNZO YA AWALI YA KIJESHI KWA KUJITOLEA

 







 Brigedia Jenerali Charles Peter Feluzi amewataka vijana waliohitmimu  mafunzo ya awali ya kijeshi ya jeshi la kujenga Taifa (JKT)  kuwa wazalendo waaminifu na waalibifu katika kusimamia na kuijenga  nchi yao


Brigedia Jenerali Charles Feluzi ametoa rai hiyo wakati akifunga mafunzo ya awali ya kijeshi kwa mujibu wa sheria oparesheni ya miaka 60 ya Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Kikosi 843 huko Wilayani Nachingwea 

Amewataka wahitimu hao kutumia Mafunzo waliyoyapata katika kuijenga na kuilinda Nchi  kwa kuzingatia kiapo chao.

Pia amewataka kujiepusha na matumizi yasiyofaa katika mitandao ya kijamii badala yake waitumie mitandao katika kujifunza na kwa manufaa bila kuvunja sheria na Taratibu za Nchi yao.

Luteni Kanali Nyagalu  Malecela ni mkuu wa kikosi cha 843 Nachingwea amesema vijana hao wakiwa kambini hapo kwa majuma 16  wameweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo mafunzo ya awali ya kijeshi na kuwajenga vijana hao kuwa wakakamavu pamoja na wazalendo

Awali akitoa salamu za Wilaya katibu tawala wa wilaya ya Nachingwea Haji Mabruck Balozi aliwasihi wahitimu kuendelea kujiendeleza kimasomo.

" ni kwa kupitia Elimu kijana unaweza kuwa Meneja wa Benk, Mkuu wa kikosi, Mbunge , Waziri na Hata Rais hivyo niwasihi vijana kujiendeleza kimasomo ili mfikie malengo yenu" alisema Balozi.

Nao baadhi ya wahitimu  wakaeleza umuhimu wa mafunzo hayo sambamba na kuwasihi vijana wengine kujiunga na jeshi hilo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS