Vijana wametakiwa kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii ili kuepuka madhara yanayoweza patikana kutokana na matumizi mabaya huku wakiendelea kuwa na uzalendo kwa nchi yao ikiwemo kuilinda amani iliyopo kwa kufanya kwa kuwa mfano mzuri wa kuigwa
Hayo yameelezwa na Mgeni rasmi Brigedia Jenerali Charles Feluzi wakati wa kufunga mafunzo ya awali katika Kikosi 843 JK wilayani Nachingwea mkoani Lindi ambapo amewataka vijana hao waliohitimu Mafunzo kujiepusha na matumizi kabaya ya mitandao ya kijamii kutokana na utandawazi uliopo .
Awali akiwasilisha taarifa ya mafunzo mkuu wa Kikosi 843JK Nachingwea Mkuu wa kikosi Luteni Kanali Nyagalu Michael Malecela amesema mafunzo hayo ya awali kwa vijana hao wa kujitolea yamefanyika kwa muda wa miezi minne huku akiwaasa juu ya kuwa wazalendo pamoja na kuendelea kuwa vijana bora kwa kutojihusisha na vitendo viovu.
Kwa upande wake katibu tawala wilaya ya Nachingwea Haji Mbarouk Balozi aliwataka vijana kutumia fursa ya mitandao ya kijamii kwa faida na manufaa yao na sio kutumia vibaya mitandao hiyo
Baadhi ya vijana waliomaliza Mafunzo ya awali wamemshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuwapatia fursa mbalimbali hasa ya kupata mafunzo hayo kwani yamewaongezea ujuzi na kuwafanya kuwa wazalendo katika nchi yao.
Jumla ya vijana 562 wa kujitolea wamehitimu Mafunzo ya awali katika kikosi 845JKT Itaka na kuwafanya kuingia awamu ya pili ya kupata mafunzo mengine.
0 Comments