WAZIRI WA UJENZI INNOCENT BASHUNGWA
Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima app Dodoma
WAZIRI wa Ujenzi Innocent Bashungwa amesema kuwa ujenzi wa barabara ya Dodoma – Iringa (km 260), ujenzi kwa kiwango cha lami wa mita 450 za Barabara ya Mchepuo wa Iringa (km 7.3) na ujenzi wa madaraja madogo 7 umekamilika, taratibu za manunuzi ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa sehemu iliyobaki ya Igumbilo – Tumaini Jct (km 6.85) kwa kiwango cha lami zinaendelea.
Ameyasema hayo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akiwasilisha Bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
Aidha, amesema kazi za uimarishaji wa matabaka ya barabara katika barabara ya Iringa – Dodoma (km264) zinaendelea kwa awamu ambapo hadi Aprili, 2024 jumla ya km 21.3 zimekamilika na uimarishaji wake.
Vilevile Waziri Bashungwa amesema,manunuzi ya kumpata Mkandarasi wa ujenzi wa barabara ya Iringa – Pawaga (km 71.93); sehemuya Pawaga Jct – Ikonongo (km 5) na Itundu –Ilolo Mpya (km 20) kwa kiwango cha lami zinaendelea.
katika mwaka wa fedha 2023/24 Wizara kupitia Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa nyumba na majengo ya Serikali.
Mheshimiwa Spika, "Hadi Aprili, 2024, Awamu ya I ya ujenzi wa nyumba 150 za watumishi jijini Dodoma, imekamilika na utekelezaji wa Awamu ya II umefikia asilimia 15," Amesema Ujenzi wa Ghorofa za Watumishi wa Umma katika eneo la Magomeni Kota Awamu ya II “Block B” umefikia asilimia 96.
Aidha amesema, ujenzi wa Ghorofa za Watumishi wa Umma za Temeke Kota Jijini Dar es Salaam umefikia asilimia 33 na Ghana kota “Block II”, Jijini Mwanza umefikia asilimia 7.
Vilevile, ujenzi wa jengo la Ofisi za Wizara za Ujenzi na Uchukuzi katika Mji wa Serikali - Mtumba jijini Dodoma umefikia asilimia 73.
Mheshimiwa Spika," Katika mradi wa ukarabati wa nyumba 40 za Viongozi jijini Dodomauliohusisha nyumba tano (5), utekelezaji unaendelea na hadi Aprili, 2024 nyumba mbili (2) zimekarabatiwa kikamilifu na tatu (3) zinaendelea kukarabatiwa, " Amesema Waziri Bashungwa.
Ameeleza kuwa, Mradi wa ukarabati wa nyumba 30 za Viongozi mikoani, utekelezaji unaendelea na hadi Aprili, 2024 ukarabati wa nyumba moja (1) umekamilika na nyumba tatu (3) unaendelea.
Aidha, ukarabati wa nyumba zilizokuwa zinamilikiwa na TAMISEMI katika mikoa 20 zilizohamishiwa TBA utekelezaji ulianza kwa nyumba tisa (9) zilizopo mkoani Singida ambapo hadi Aprili, 2024 ukarabati umefikia asilimia 85.
Mheshimiwa Spika, "Katika mwaka wa fedha 2024/25, Wizara ya Ujenzi inaomba kuidhinishiwa jumla ya Shilingi 1,769,296,152,000.00 kwa ajili ya matumizi ya Kawaida na utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo, " Ameeleza.
Amesema Kati ya fedha hizo,Shilingi81,407,438,000.00 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida ya Wizara na Taasisi na Shilingi 1,687,888,714,000.00 kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo.
Kati ya fedha za Matumizi ya Kawaida, Shilingi 76,588,233,000.00 ni za Mishahara ya Watumishi na Shilingi 4,819,205,000.00 ni za
Matumizi Mengineyo.
Bajeti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo inajumuisha fedha za ndani Shilingi 1,141,803,989,000.00 na fedha za nje ni Shilingi 546,084,725,000.00.
Fedha za ndani zinajumuisha Shilingi 599,756,467,800.00 kutoka Mfuko wa Barabara na Shilingi 542,047,521,200.00 ni fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali.
0 Comments