Header Ads Widget

SERIKALI KUONGEZA KODI MAFUTA YA KULA YANAYOTOKA NJE

 

Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA 


SERIKALI imepanga kuongeza kodi kwa mafuta ya kula yanayoagizwa nje ya nchi katika bajeti ya 2024/2025 kwa lengo la kulinda viwanda vinavyozisha mafuta hayo hapa nchini.


Waziri wa Kilimo,Hussein Bashe, amesema hayo leo (Mei 31, 2024) baada ya kupigiwa simu na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi,ambaye alimpigia kufuatia wananchi wa kijiji  cha Itaja jimbo la Singida Kaskazini kulalamikia ukosefu wa soko la uhakika kwa ajili ya mazao wanayozalisha.


"Mheshimiwa Katibu katika bajeti kuu ya serikali ambayo inatarajia kusomwa bungeni hivi karibuni serikali itaongeza kodi katika mafuta ya kula yanayoingizwa nchini kutoka nje ili kulinda mafuta ya ndani,"amesema.


Dk. Nchimbi amemwagiza waziri Bashe kuhakikisha soko la vitunguu linajengwa katika jimbo la Singida Kaskazini kama wananchi walivyoomba ambapo Bashe alimhakikishia Katibu Mkuu wa CCM kwamba soko hilo litajengwa kabla ya 2025 na kwamba wiki ijayo atatuma wataalam jimboni humo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI