Na WILLIUM PAUL.
VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mwanza, Michael Lushinge Masanja (MNEC) wamemkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi Rehema Sombi Omary (MNEC) katika ofisi za CCM za Mkoa wa Mwanza na kumsomea taarifa fupi ya hali ya kisiasa, uhai wa chama na kazi za Jumuiya ya UVCCM.
Rehema Sombi amefika Mkoani Mwanza ambapo amealikwa kuwa Mgeni Rasmi Kwenye Mahafali ya Seneti Vyuo na Vyuo Vikuu mkoa wa Mwanza yanayotarajiwa kufanyika tarehe 19 Mei 2024.
0 Comments