Header Ads Widget

MAJALIWA MGENI RASMI KONGAMANO LA WAANDISHI WA HABARI ZA MITANDAONI ..

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Mwenyekiti JUMKITA Shaaban Matwebe

JUMIKITA (Jumuiya ya Mitandao ya Kijamii Tanzania) kwa kushirikiana na TAHLISO

(Shirikisho la Serikali za Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Tanzania) inaandaa Kongamano la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii nchini litakalofanyika tarehe 20/5/2024 kwenye ukumbi wa Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam.

JUMIKITA inapenda kuutaarifu umma kuwa, Kongamano hilo litakuwa na dhima kuu ya kujadili undishi wa habari kupitia mitandao ya kijamiii pamoja na upashanaji wa habari kupitia mitandao hiyo. Pamoja na dhima hiyo kuu, Kongamano hilo litajadili mafanikio ya miaka mitatu ya serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan ikia ni pamoja na maadhimisho ya siku ya uhuru wa habari duniani

Aidha, Kongamano hilo linalotarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 500, litaongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa

Mada mbalimbali zitajadiliwa ikiwa ni pamoja na mitandao ya kijamii na uzalendo, fursa zilizopo kwenye tasnia hii, mafanikio na changamoto ili kutoa mchango wa kiundeshaji kwa wadau kupitia JUMIKITA na mapendekezo yatakayosaidia serikali kwenye uratibu wa sera za jinsi ya kuunganisha sayansi ya uchumi wa taarifa (information economics) na uchumi wa taarifa (information economy)

JUMIKITA inawakaribisha wote kwenye Kongamano hili muhimu kwa ustawi wa nchi yetu.


Mawasiliano

Mwenyekiti JUMKITA~Shaaban Matwebe~0717073534

Sekretarieti~

Dickson Frank Mushi~0686379370

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI