Header Ads Widget

MBUNGE ABOOD AJITOLEA MADAWATI YA TSH MILIONI 28 JIMBONI MOROGORO

 


Na Ashton Balaigwa,MOROGORO

MBUNGE wa Jimbo la Morogoro Mjini(CCM) AbdulAzizi Abood,ametoa msaada wa Madawati yenye thamani ya Shilingi Milioni 28 kwa Shule ya Sekondari ya Mazimbu iliyopo Manispaa ya Morogoro.

 Hatua ya Mbunge Abood  kuamua  kutoa madawati hayo inatokana na ziara yake  aliyoifanya ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa shule mpya zilizojengwa na Halmashauri na nguvu za wananchi na fedha za Serikali kuu maarufu kama fedha za UVIKO 19 na kubaini kuwepo kwa wanafunzi wakikaa chini.

Akizungumza wakati akikabidhi Madawati hayo ambayo ni meza ni Meza 310 pamoja na viti 310,Abood alisema ameamua kutoa msaada huo ili  kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan katika kutatua changamoto za elimu hapa nchini.

“ Rais wetu ,Mama yetu Samia Suluhu Hassan,amefanya juhudi kubwa sana katika suala la elimu ametafuta fedha na kujenga madarasa ,sasa changamoto nyingine la upungufu wa madawati lazima tumsaidie na kumuunga mkono hivyo nimeamua kusaidia madawati” alisema Mbunge  Abood.

Mbunge huyo  alifafanua kuwa, ujenzi wa madarasa ni jambo moja na kuunga mkono jitihada za za Rais Samia  kwa kutoa  madawati ili watoto waweza kupata hari ya kusoma ni jambo lingine, hivyo kama Mbunge ameliona hilo na kuamua kutengeneza Meza pamoja na Viti vyenye uwezo wa kutosha kuhudumia wanafunzi na madarasa zaidi ya sita  kwa lengo la kuwafanya walimu wafundishe vema.
“Nilikuja hapa katika ziara yangu ya kushtukiza na nikakutana na changamoto ya madawati, nimekuta wanafunzi wanakaa chini, nilihisi nina jambo naweza fanya, na ndipo nilipoahidi kuwa nitatoa madawati ili kuondoa changamoto na hatimaye watoto wetu waweze kukaa kwa utulivu, leo nimetekeleza” alisema Mbunge Abood.

Naye Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, ambaye  ni Diwani wa Kata ya Mazimbu Pascal Kihanga alisema  kuwa, Mbunge Abood  amekuwa msaada mkubwa ndani na nje ya Baraza la Madiwani la Halmashauri hiyo na kupelekea kutengeneza madawati zaidi ya 5000 ambayo yanatarajiwa kusambazwa katika Shule zote mpya zilizopo kwenye Manispaa hiyo ili kumaliza kabisa tatizo hilo.

Akiwakilisha wazazi wenye watoto wanaosoma  Shule hiyo ya Sekondari ya Mazimbu,Hezron Njau alipongeza jitihada za Mbunge huyo kwa kutatua changamoto ya upungufu wa  madawati ambayo ilisababisha wanafunzi kukaa chini.

Mwisho

MAELEZO YA PICHA

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini AbdulAziz Abood katikati mwenye miwani,akiwa pamoja na Walimu wa Shule ya Sekondari ya Mazimbu Manispaa ya Morogoro,baada ya kukabidhi madawati yenye thamani ya sh milioni 28 ili kutatua changamoto ya watoto waliokuwa wakikaa chini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI