Mkoa wa lindi umezindua mpango mkakati wa Elimu wa mwaka 2024 wenye lengo la kukabiliana na kuondoa changamoto 15.
Uzinduzi huo umefanyika jana mei 5 2024 katika viwanja vya shule ya Likangara huko Wilayani Ruangwa ulienda sambamba na utoaji wa zawadi kwa walimu , wanafunzi na shule zilizofanya vizuri katika mitihani na pimaji za kitaifa .
Akizungumza kabla ya Uzinduzi huo Mkuu wa mkoa wa Lindi Bi.Zainab Telack alisema toka Mkoa huo umeanza kuweka mikakati ya Elimu kila mwaka Mkoa umeendelea kupata matokeo mazuri katika mitihani na pimaji mbalimbali za kitaifa
Amesema miongo mwa mafanukio hayo ni Mkoa huo kuendelea kung'ara katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha sita kwa miaka mitano mfululizo 2021-2023 kwa kufaulisha wanafunzo wote kwa asilimia 100%
"Mwaka jana tumeweza kufanikisha kuondoa daraja la nne, katika wanafunzi wetu wa kidato cha sita. Kama hiyo haitoshi Mkoa wetu pia umeweza kupandisha madaraja kutoka daraja la kwanza wanafunzi 645 mpaka 678" alisema Telack
Hata hivyo Telack aliwapongeza wazazi, walimu na wanafunzi kwa mashirikiano yao katika kuinua kiwango cha Elimu katika Mkoa huo.
Kwa upande wake Afisa Elimu wa Mkoa huo Joseph Mabeyo amesema mpango huo mkakati wa Elimu mwaka 2024 umezingatia mambo mbali mbali ikiwemo sera ya Elimu namba 25 ya mwaka 1978 na marekebisho yake namba 10 ya mwaka 2002 sera ya elimu na mafunzo ya mwaka 2024 nyaraka na miongozo mbalimbali ya Serikali . Maelekezo ya viongozi na muelekeo wa serikali katika mahitaji halisi ya mkoa huo
"Kwa kuzingatia vigezo hivyo mpango huu umejikita kutatua changamoto 15 ambapo kila ngazi ya usimamizi wa Elimu imepewa majukumu ya kusimamia na muda wa utekelezaji "
Baadhi ya walimu na wazazi wamesifu jitihada zinazofanywa na Mkoa huo katika upandishaji wa Elimu kwa wanafunzi huku wakieleza kuwa utolewaji wa tunzo unaenda kuongeza hali katika kupandisja alama za ufaulu kwa wanafunzi.
0 Comments