NA WILLIUM PAUL,
MBUNGE wa Jimbo la Moshi Vijijini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro, Prof. Patrick Ndakidemi ameendelea kuwapambania wananchi wa jimbo hilo katika kuwaletea maendeleo ambapo ameibana serikali kumaliza ujenzi wa hospitali ya halmashauri ya Moshi inayojengwa kata ya Mabogini.
Akiuliza swali la nyongeza Mbunge Prof. Ndakidemi alihoji Je? Serikali ina mipango gani ya kumalizia ujenzi wa Hospitali ya wilaya inayojengwa Mabogini katika jimbo la Moshi vijijini.
Akijibu swali hilo Naibu Waziri Ofisi ya Rais na Serikali za Mitaa Tamisemi, Zainab Katimba alimuhakikisha Mbunge huyo kuwa hospitali hiyo itajengwa.
Zainab alisema kuwa, katika mwaka wa fedha 2024/25 Serikali imetenga Bilioni 43.84 kwa ajili ya kukamilisha miradi viporo vya hospitali za halmashauri na kumkakikishi kuwa hospitali hiyo ni miongoni mwa hospitali hizo.
Mwisho...
0 Comments