Header Ads Widget

AFRIKA MASHARIKI : MAFURIKO YAUA WATU ZAIDI YA 235 NA WENGINE 234,000 KUPOTEZA MAKAZI.

 


Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) jana ilisema karibu watu 750,000 waliathiriwa na mafuriko katika Afrika Mashariki, huku watu 234,000 wakipoteza makazi yao na zaidi ya 236 wamefariki ambapo Kenya pekee idadi ya waliofariki ni zaidi ya 229.

OCHA pia ilisema Kenya iliripoti watu zaidi ya 285,000 wameathirika nchini kote. Ofisi hiyo ilisema kuwa Umoja wa Mataifa na washirika wake wanaunga mkono hatua zinazochukuliwa na serikali na wametoa misaada ya maji safi na vifaa vya matibabu kwa watu 126,000, na kutoa chakula na pesa kwa watu 31,000, watu zaidi 5,000 wamepata huduma za afya, na karibu watu 26,000 wamepata makazi ya muda.

Kwa mujibu wa OCHA, nchini Somalia watu zaidi 160,000 waliathiriwa na mafuriko, huku zaidi ya 37,000 wakihamishwa makazi yao. Mafuriko yamesababisha vifo vya watoto saba tangu tarehe 19 mwezi Aprili, huku majimbo ya Hirshabelle, Jubaland na Kusini Magharibi yakiwa yameathiriwa zaidi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS