Header Ads Widget

WILAYA YA NACHINGWEA YAPANDA MITI ZAIDI YA 100,000 WIKI YA MUUNGANO

Na mwanahabari wetu, Lindi MAtukio Daima App,

     MKUU WA WILAYA YA NACHINGWEA MOHAMED MOYO AKIPANDA MTI
   


UONGOZI wa wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi umeadhimisha miaka 60 ya Muungano kwa kupanda zaidi ya miti 100,000 katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ikiwa na lengo la kuendelea kutunza mazingira na vyanzo vya maji.
 

Akizungumza mara baada ya zoezi la upandaji miti, mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wananchi wa Nachingwea watapanda zaidi ya miti 100,000 kwenye maeneo mbalimbali.


Moyo alisema kuwa ilikuwa na mazingira mazuri na kutunza vyanzo vya maji lazima kila mwananchi anapaswa kupanda miti kila anapokataa mti laki kupanda miti kwenye vyanzo vya maji ili kutunza vyanzo hivyo.
 


Katika hatua nyingine, amewataka wananchi kuacha mara moja tabia ya kukata miti hovyo katika wilaya hiyo na atakayebainika utachukuliwa sheria kwa mujibu wa katiba ya nchi inavyosema.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS