Header Ads Widget

WAZIRI ULEGA AHIMIZA UWEKEZAJI WA MITAJI KATIKA SEKTA ZA MIFUGO NA UVUVI

 


Na Thobias Mwanakatwe

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega,  amesema sekta za mifugo na uvuvi zinaweza kuwa na tija kubwa zaidi kama taasisi za kifedha zitaendelea kuwekeza mitaji katika sekta hiyo.


Akizungumza leo  wakati akifafanua baadhi ya hoja za wadau wa Kongamano la Uwekezaji la CRDB lililopewa jina la “Uwekezaji Day 2024”linalofanyika jijini Dar es Salaam, amesema uwekezaji ukifanyika katika sekta ya  mifugo na uvuvi zitaweza kuzalisha kwa tija na hivyo kuchangia vyema kwenye pato la Taifa.


Amesema sekta za mifugo na uvuvi zinaweza kuwa na  tija kubwa katika uchumi wa taifa hivyo ni muhimu taasisi za kifedha ikiwemo CRDB kuendelea kuwekeza mitaji ili kuinua wadau wanaojishughulisha na sekta hizo.


“Nawapongeza CRDB kwa kuaandaa Kongamano hili kubwa la uwekezaji day, ombi langu kwenu, jukwaa hili liwe chachu ya kubadili sekta hizi za uzalishaji kwa kuongeza mitaji ili kuchechemua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla”, amesema Ulega.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS