Header Ads Widget

NJOMBE: WATUMISHI WA UMMA WAONYWA KUTOA HUDUMA KWA NJIA YA RUSHWA

 

Na Gabriel Kilamlya, Matukio Daima app njombe.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Njombe imewaonya baadhi ya watumishi wa Umma wanaojihusisha na vitendo vya Rushwa kwani imebainika kuwapo kwa wanaotoa huduma mpaka wahongwe.

Akizungumza na vyombo vya habari wakati akiwasilisha ripoti ya utendaji kazi ya miezi mitatu Kamanda wa Takukuru mkoa wa Njombe Cassim Ephrem amesema baadhi ya watendaji wamekamatwa wakipokea rushwa ili watoe huduma kwa wananchi jambo ambalo haliwezi kufumbiwa macho.

Aidha Kamanda Cassim amesema tayari kesi mbalimbali za watumishi waliokutwa wakijihusisha na vitendo vya kushawishi na kupokea rushwa zipo mahakamani na kwamba ni aibu kwa mtumishi wa Umma kujihusisha na vitendo hivyo.

Pia amewaonya baadhi ya Polisi wanaopokea fedha kwa wananchi isivyohalali hususani katika makosa ya  barabarani tena kiasi kidogo cha shilingi elfu moja au elfu mbili kitendo kinachoweza kumdhalilisha ili hali analipwa mshahara unaotokana na kodi za wananchi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS