Header Ads Widget

WAANDISHI WAMTUNUKU TUZO YA KINARA WA UCHUMI WA BULUU RAIS SAMIA

 


Mkurugenzi Mtendaji wa  chama hicho Bwana Edwin Soko alikabidhi tuzo hiyo kwenye hafla ya jioni ya uchumi wa buluu iliyofanyika Jijini Mwanza jana, Soko alisema kuwa wamemkabidhi tuzo hiyo Rais kutokana na utendaji wake wa umahiri kwenye sekta ya uvuvi na uchumi wa buluu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Muhamed  Mtanda akipokea tuzo kwa niaba ya Rais alisema kuwa, Rais amekuwa akihimiza sana kuchangamkia fursa  za uchumi wa buluu pamoja na kuwekeA fedha nyingi kwenye zana za uvuvi ili sekta hiyo iweze kuchangia kwa kiasi uchumi wa Nchi.

Pia Chama hicho  kimetoa tuzo kwa Naibu Waziri Mkuu  na Waziri wa Nishati Doto Mashaka Biteko ya kuwa kinara wa usimamiaji wa Bwawa la Kufua umeme la Mwalimu Nyerere ikiwa ni alama ya kuchangamkia fursa za uchumi wa buluu.

Pia TMFD imetoa tuzo kwa mshindi wa picha bora ya Mwaka  2023 - 2024 yenye maudhui ya Uchumi wa buluu, Nestory Kishatu,.

TMFD imekuwa ikifanya kazi mbalimbali ikiwemo kuwajengea uwezo waandishi wa habari katika eneo la uvuvi kwa kuwapa  mafunzo ili waweze kuandika habari kwa uvuvi kwa usahihi.



Hafla hiyo ilifanyika kwenye ukumbi wa kipepeo the breeze na kuhudhuriwa na viongozi wa serikali, AZAKI waandishi wa habari, wafanyabiashara wa dogo na wakubwa wa sekta ya uvuvi.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI