Menejimenti pamoja na viongozi kutoka idara na Vitengo mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba leo hii wamehitimisha mafunzo ya siku 7 ya ‘BASIC HOSPITAL MANAGEMENT’ yaliyoendeshwa na wataalamu kutoka Wizara ya Afya wakishirikiana na wataalamu kutoka Taasisi ya Afya ya Msingi Iringa (PHIC0) yakiwa na lengo la kukumbushana mambo mbalimbali ya kiutawala na kiutendaji.
Akitoa shukrani zake kwa wakufunzi hao baada ya kutamatika kwa mafunzo hayo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba Dr. Museleta Nyakiroto amewashukuru wataalamu hayo kwa kukubari ombi lao la kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo kwa wiongozi wote wa BRRH.
“Kwaniaba ya uongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba natoa shukurani zangu nyingi kwa Wizara ya Afya pamoja na nyinyi wataalamu kwa kukubali ombi letu la kutupatia mafunzo haya hapa BRRH, kiukweli tumejifunza na kukumbushwa mambo mengi ya kiuongozi na kiutawala ni hakika yangu kuwa yatatusaidia sana katika utendaji wetu na hutoaji huduma bora kwa wananchi”
Aidha amewasihi viongozi wenzake kuyatumia vyema maarifa waliyopatiwa na wataalamu hao katika kutimiza majukumu yao ya kiuongozi na utendaji kazi kwa kuzingatia sera na miongozo ya Afya.
Naye mwakilishi kutoka Wizara ya Afya Idara ya Tiba, Glory Laizer amewashukuru viongozi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba kwa upendo, umoja, utulivu na ukalimu waliouonyesha viongozi hao katika kipindi cha siku 7 za mafunzo hayo huku akuwashi kuyazingatia na kuyafanyia kazi yote waliyofundishwa ili kuweza kupiga hatua katika kutimiza majukumu yao.
“Tumejionea mambo mazuri ambayo hatukutegemea hasa kwenye suala la umoja, ukalimu, utayari wa kujifunza na upendo. Kupitia haya hata sisi tumeyabeba, lakini mkumbuke kuyaishi na kuyafanyia kazi mambo yote mliyojifunza ili kuweze kupiga hatua zaidi hususani katika suala la uongozi na utawala na uboreshaji wa huduma”
0 Comments