Header Ads Widget

WATANZANIA WATAKIWA KUIPIGIA NGORONGORO KURA ILI KUSHINDA TUZO HII

 


 NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA.

Mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro imezindua rasmi zoezi la upigaji kura ili kuiwezesha mamlaka hiyo kushinda katika tuzo ya kuwa kivutio bora cha utalii barani Afrika jambo ambalo litaifanya Tanzania kuendelea kuaminika na kuweza kuingiza watalii wengi zaidi na kukuza uchumi.



Akiongea na waandishi wa habari Aprili 28,2024 Kaimu Kamishna  wa uhifadhi wa mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro Victoria Shayo alisema kuwa Aprili 4,2024 mtandao wa World Travel Award ilitangaza kuiteua  kwa mara nyingine  mamlaka hiyo kuwania tuzo ya kivutio bora cha utalii barani  Afrika ( African lead tourist atraction) ambapo kwa mwaka 2023 waliweza kuwania tuzo hiyo na kushinda.



“Mwaka huu tena tunashindania tuzo hiyo kwahiyo  leo April 28 NCAA tunazindua rasmi upigaji kura ambao utaenda na kaulimbiu isemayo 'YOU VOTE ,WE WIN' kwa maana ya kwamba kura yako ushindi wetu,” Alisema kamishna Shayo


Alieleza kuwa eneo la Ngorongiro pamoja na kuwa kivutio bora cha utalii barani Afrika  kwa mwaka 2023, lina sifa tatu za umoja wa mataifa na ni hifadhi pekee yenye hadhi hiyo kusini mwa jangwa la sahara na ya pili kwa hadhi hiyo bara la Afrika.


Alifafanua kuwa dirisha la upigaji kura limefungulia tangua April 2 ambapo zoezi litaendelea hadi septemba 8,2024 hivyo amewaomba watanzania wote kutumia muda isiozidi dakika mbili kupigia kura eneo la hifadhi ya Ngorongoro ili kuweza kushinda tuzo hiyo.



“Kwa umoja wetu watanzania  tukipiga kura tutashinda, na itasaidia  kuingiza watalii wengi zaidi kwasababu itaendelea kuaminika  jambo litakalotufanya tuingize fedha za kigeni na kukuza uchumi wa nchi yetu ikiwa ni pamoja na kuendelea kuitangaza nchi yetu kimataifa kwasababu katika  kinyang'anyiro hichi tunashindana na nchi zingine Afrika ambazo ni Afrika Kusini, Botswana, Misri,pamoja na Malawi,” Alieleza 



Aidha alifafanua kuwa  kwa mwaka 2022/2023 wameweza kuingiza wageni  laki 750 huku mapato yakiwa  ni bilioni 171  ambapo kwa mwaka huu wa 2023/2024 hadi kufikia mwezi March wameshapokea wageni laki 752 na mafanikio hayo yanachangiwa na Royal tour ambayo Rais Samia aliifanya kuitangaza nchi vizuri na hadi kufikia Disemba mwaka jana mapato yalikuwa ni bilioni 123 ambalo ni ongezeke la asilimia 13 kulinganisha na mwaka uliopita.


“Mpaka kuisha kwa mwaka huu wa fedha tunatarajia kuingiza wageni 1,000,000 lakini pia kuongezeka kwa mapato yetu hadi kufikia bilioni 200 kwahiyo ni eneo ambalo tukiendelea kulitangaza kwa kulipigia kura kama nchi tutaendelea kunufaika zaidi,” Alisema.


Hata hivyo alieleza kuwa eneo la Ngorongoro lina ukubwa wa kilomita za mraba 8,292 ambapo kuna vivutio mbalimbali ikiwemo msitu wa nyanda za juu Kaskazini, creter, uhifadhi wa mambo kale( Olduvai, Laitole) Mlima wa tatu kwa urefu Tanzania Lolmasin, pamoja na creter nyingine mbili ya Embakai na  Olmoti, ikiwa ni pamoja na Nasera rock,Endoro na nyinginezo nyingi.


Kwa upande wake Peter Makutian Afisa utaliu mkuu wa mamlaka hiyo alisema kuwa kilichofanya wakashinda 2023 ni kutokana na eneo hilo kuwa na vivutio lukuki pamija na kushiriki kwa watanzania wengi katika upigaji wa kura pammojq na wataalamu wa masuala ya utalii hivyo tunatoa wito tena kwa watanzani kuweza kuipigia yena Ngorongoro kura.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI