Header Ads Widget

TRILION 11.4 KUTOA AJIRA LUKUKI KIGOMA

 

Shekhe wa mkoa Kigoma Alhaji Hassan Iddi Kiburwa

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Kiasi cha shilingi trilioni 11.4  kilichotolewa na serikali kwa ajiili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya kimkakati mkoani Kigoma zinaelezwa kutengeneza ajira kubwa za muda na za kudumu hivyo MKUU wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye amewataka wananchi wa mkoa Kigoma kuchangamkia fursa hizo za ajira.

 Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye ametoa kauli hiyo akitoa hutuba wakati wa baraza la Eid El Fitr lililofanyika kwenye viwanja vya matofalini Ujiji mjini Kigoma ambapo amewataka viongozi na waumini wa dini ya kiislam mkoani Kigoma kuchangamkia fursa hizo za ajira.

 Andengenye alisema kuwa serikali kwa sasa imeanza kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati inayolenga kuufungua mkoa na kuufanya kuwa wa kimkakati kiuchumi na kwamba utekelezaji wa miradi hiyo inahitaji watenda kazi wakiwemo wa kazi za kitaalam na zile zisizo za kitaalam hivyo wananchi wa mkoa huo wakiwemo waumini hao wa kiislam kuwa karibu na miradi hiyo ili waweze kupata fursa hizo za ajira.

Mkuu wa mkoa Kigoma Thobias Andengenye (aliyesimama) akizungumza katika Baraza la Eid El Fitr lililofanyika viwanja vya matofalini Ujiji mjini Kigoma

Aliitaja miradi hiyo kuwa ni Pamoja na miradi ya umeme wa gridi ya Taifa, ujenzi wa kiwanda cha meli, ujenzi wa meli mpya mbili, upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kigoma, ujenzi wa reli iendayo kasi (SGR) huku miradi ya miundo mbinu ya barabara, elimu, afya ikiendelea kutekelezwa kwa kiasi kikubwa cha fedha.

 Awali akizungumza katika baraza hilo la Eid El Fitr Shekhe wa mkoa Kigoma,Alhaji Hassan Iddi Kiburwa alisema kuwa viongozi wa dini mkoani humo wanaridhishwa na ushiriano uliopo baina ya serikali na madhehebu ya dini mkoani humo hivyo wako tayari kushiriki kwenye michakato ya miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea.

Shekhe Kiburwa alisema kuwa wanazo taarifa za kupelekwa mkoani humo kwa kiasi kikubwa cha pesa na Raisi Samia Suluhu Hassan hivyo wao viongozi wa dini na waumini wao wako tayari kushiriki kwa hali na mali katika utekelezaji wa miradi hiyo kwani inagusa Maisha ya wananchi wa mkoa huo.

 


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI