Header Ads Widget

TAWA YAKABIDHI MSAADA WA MILIONI 20 KWA WAATHIRIKA WA MAFURIKO PWANI

 



Serikali kupitia mamlaka ya wanyama pori Tanzania TAWA imekabidhi misaada mbalimbali ya kibinadamu ikiwemo Magodoro 186 , tani 6.5 za  Unga  , kilo 666 za Mharage pamoja na Boti la uokozi kwa waathirika wa mafuriko Wilayani Rufiji Mkoani pwani vyenye thamani ya milioni 20.

Akipokea msaada huo Mkuu wa Mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge Ameendelea kumshukuru Rais samia kupitia wadau na taasisi mbalimbali wanaofika katika eneo hilo na kutoa misaada .

amesema kuwa  hatua ya Tawa kutoa misaada hiyo  ni ishara kubwa ya kutambua uwepo wao katika eneo hilo katikashuguli mbalimbali 

Hata hivyo Rc kunenge  amesema kuwa msaada huo umefika wakati muafaka ambapo waathirika bado wanahitaji msaada pamoja na kuahidi  kufikisha msaada huo kwa walengwa waliokusudiwa 

Kamishina wa uhifadhi wa mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA kanda ya kusini  Mashariki Abraham Jullu amesema vitu hivyo walivyokabidhi leo vimetokana na ujirani mwema kati ya mamlaka hiyo  na wananchi wa Rufiji katika shughuli zao za uhifadhi 

" TAWA tupo hapa kwa sababu Mkoa wa pwani katika Wilaya ya Rufiji tuna pori letu la akiba la serous  kupitia kanda ya kingupira hivyo tofauti na watanzania ambao tupo hapa kuja kuungana na wenzetu na kuungana na wewe lakini pia waliopata majanga haya ni watu wetu wa karibu na ni majirani zetu katika uhifadhi hivyo matatizo yao na raha yao na sisi inatuhusu"

Kwa upande wake Mjumbe kamati ya utawala katiba na sheria inayosimamia Wizara ya Ofisi ya Waziri Mkuu sera, Bunge na uratibu Dkt . Alice kaijage ni ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali kwa namna ambavyo inashughulika na wananchi hao walioathiriwa na mafuriko 






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS