NA WILLIUM PAUL, SAME.
SERIKALI mkoani Kilimanjaro kupitia wakala wa barabara nchini (TANROADS) imekarabati barabara ya ya Mwembe-Myamba -Ndungu yenye urefu kilomita 90.19 kwa kiwango cha Changarawe kwa thamani ya bilioni 1.6.
Mapema mwaka jana kupitia mvua za Eli-Nino barabara hiyo ilikata mawasiliano baada maporomoko ya ngema na Miamba(mawe Makubwa) kutoka upande wa milimani.
Akizungumza mkuu wa mkoa Kilimanjaro Nurdin Babu katika ziara ya kawaida ya kukagua miundombinu kutokana na mvua zinazoendelea hapa nchini
"Hii barabarani ni muhimu kwa maslahi mapana ya wananchi wa wilaya ya Same hasa wakulima wa tangawizi hivyo ililazimika kurudisha mawasiliano kwa haraka zaidi..
Mimi mwenyewe nilikuja nikakwama huku nikalazimika kutumia njia mbadala ambayo ni mbali na sio wananchi wote wanaweza kufika kwenye njia hiyo,"Alisema Babu
Aidha Mkuu wa kitengo cha matengenezo ya barabara TANROADS mkoa wa Kilimanjaro, Mhandisi Benitho Nikodemu alisema maeneo 18 ya barabara hiyo yalikuwa mito inapita na makorongo jambo ambalo yalisabisha kumeguka na ngema kuanguka barabarani.
Mhandisi alisema matengenezo yaliyofanyika ni pamoja na kuchonga barabara (Heavy Grading) urefu wa kilomita15 na kuweka changarawe na kupasua miamba .
Alisema "Tulipanua barabara maeneo finyu yaliyotokea ufa kwenye tuta la barabara kujaza mawe makubwa(Rock boulders)maeneo yaliyokatika na kujenga mitaro na kuta za mawe na kazi hii ilifanyika kwa haraka kutokana na mkandarasi kuwa na vifaa vingi na vya kuaminika,"alisema Mhandisi.
Aidha mkandarasi anayefanya matengenezo katika barabara hiyo mhandisi Baliunmn Mathias kutoka kampuni JP Traders alisema mradi huo umekamilika kwa asilimia 95 na kuomba mwezi moja ili kumalizia maeneo yaliyobakia na kufanya marekebisho watakayomaliza.
"Kwa sisi ni kama tumemaliza kwa sasa tunasubiri kukamilisha asilimia 5 iliyobaki pamoja na kupokea maelekezo tutakayoelekeza ili kuongeza ufanisi,"alisema.
Mwisho..
0 Comments