Header Ads Widget

TAHADHARI YA MAFURIKO YATOLEWA KILOMBERO DC KYOBYA NA DED MICHUZI WAFIKA ENEO LA MTO ULIHARIBIKA

 


Mkuu wa Wilaya  ya Kilombero  mkoani Morogoro Dustan Kyobya na Mkurugenzi wa Ifakara Mji  Zahara Michuzi wamefika eneo la kingo za mto lumemo ambao umejaa sana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kuleta mafuriko kwenye makazi na taasisi za umma na binafsi.


Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi  kuchukua tahadhari mapema na kuondoka maeneo yote yaliyojaa maji.


Baadhi ya shule zimelazimika kufungwa kwa muda mpaka maji yatakapopungua



Timu za uokoaji  zimepata boti kutoka  TAWA na zinaendelea na doria ya nyumba kwa nyumba kuokoa wananchi.


Nyumba nyingi bado zimezungukwa na maji, hivyo timu za uokoaji zikiongozwa na kamanda wa zima moto wilaya kamanda Haji , Skauti wilaya, redcross wilaya na Halmashauri zinaendelea na doria za nyumba kwa nyumba kuokoa wananchi walioshindwa kutoka majumbani mwao







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS