Header Ads Widget

RC NJOMBE:MIUNDOMBINU BORA YA ELIMU IENDANE NA MATOKEO MAZURI YA KIDATO CHA SITA

 

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati wanafunzi wa kidato cha sita wakitarajia kufanya mtihani wao wa mwisho hapo mei 6 mwaka huu nchini Kote Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amewataka kujali jitihada za serikali katika uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwa kufanya vizuri.



Mtaka ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa Mount Kipengere Sekondari Wilayani Wanging'ombe alipozulu na kukagua miundombinu ya elimu pamoja na kuwatakia Kheri katika mitihani wanafunzi hao.


Awali Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Wanging'ombe Nicephorus Mgaya ambaye ni Ofisa Mipango wa Halmashauri hiyo amesema serikali imepeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa na Mabweni shuleni ili wanafunzi wasome katika mazingira rafiki.


Mkuu wa wilaya ya Wanging'ombe Claudia Kitta ametaka kuona matokeo chanya katika elimu kwa wanafunzi hao kupitia uwekezaji wa miundombinu hiyo ya elimu.


Mbele ya mkuu wa mkoa wa Njombe,baadhi ya Wanafunzi hao akiwemo Matrida Nziku na Joseph Mapunda wamekiri kuwapo kujengwa kwa miundombinu Rafiki shuleni hapo na inawasaidia kusoma katika mazingira mazuri yatakayowawezesha kufanya vyema katika masomo.


Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka anaendelea na ziara katika shule mbalimbali mkoani na kuwahamasisha wanafunzi wa kidato cha sita kwenda kufanya vizuri katika mtihani wao wa Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS