Header Ads Widget

PAUL MAKONDA MATATANI

 


Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi  ( CCM) Paul Makonda ambaye ameteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha ameripotiwa kutuhumiwa kumtishia maisha mfanyabiashara Sallah Mohammed mmiliki wa kampuni ya usafirisha mizigo ya Silent Ocean.


Kwa mujibu wa kituo cha redio cha Wasafi ambacho pia kimefanya mahojiano na Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya dar es salam, mfanyabiashara huyo ameripoti tukio hilo na kuwa mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar Es Salaam (ZCO) Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Faustine Mafwele analifahamu suala hilo.


Katika mahojiano na kituo hicho cha redio Kamanda Muliro ameonesha kutokuwa na taarifa hiyo na kuwa kama limeripotiwa tayari watalifuatilia kama ilivyo taratibu za jeshi la Polisi zinavyoelekeza.


“ Sisi utaratibu za kawaida ,yani hata wewe ukija ukasema jambo lolote,sisi kazi yetu ni kuchunguza,hatukukubalii au hatukukatalii,jukumu letu ni kuchunguza, ndo maana nimekuuliza nani amesema hivyo na ametoa taarifa hizo wapi, kwa hiyo hicho ndicho nachoweza nikakwambia tu” amesema Kamanda Muliro katika mahojiano hayo.


Mahojiano hayo yamefanyika 01 April 2024 mara baada ya kusambaa kwa taarifa za tishio hilo la Makonda dhidi ya mfanyabiashara huyo Sallah huku kukisubiriwa taarifa rasmi ya jeshi hilo ambayo ianatarajiwa kuelezea kwa kina jambo hilo.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI