NA WILLIUM PAUL, SIHA.
Akiweka jiwe msingi la mradi huo, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Godfrey Eliakimu Mzava alisema kuwa,Serikali haileti miradi ili wananchi wake waumie bali wananchi wote wapate faraja.
Mzava alisema kuwa, lengo la Mwenge wa Uhuru ni kuleta matumaini sehemu ambapo hakuna matumaini kuleta upendo mahali ambapo kunachuki kuleta heshima mahali ambapo kumejaa zarau.
Kiongozi huyo wa Mwenge aliridhia kuweka jiwe la msingi katika daraja hilo.
Awali akisoma taarifa ya ujenzi huo kwa Kiongozi huyo wa Mwenge, Mtendaji wa kijiji cha Munge, Wine Muro alisema kuwa, mradi huo utagharimu milioni 35.2 ambapo mpaka sasa wameshatumia milioni 19.3 na umefikia asilimia 96 ya ujenzi.
Naye Diwani wa viti maalum, Liliani Mollel alitumia nafasi hiyo kuishukuru serikali kwa ujenzi wa Daraja kwani wananchi walikuwa wakipata shida hasa kipindi cha mvua.
Mwisho..
0 Comments