Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MBUNGE wa jimbo la Kigoma Kaskazini Asa Makanika ametoa kiasi cha shilingi milioni tano kwa jumuiya ya wazazi katika wilaya ya Kigoma Vijijini kuweza kuanzisha mradi wa kiuchumi utakaowezesha jumuiya hiyo kupata fedha zitakazokuwa zikigharamia mambo mbalimbali ya jumuiya badala ya kuwa ombaomba
Makanika alisema hayo akizungumza na viongozi na wajumbe wa baraza la Wazazi wilaya ya Kigoma vijijini na kusema kuwa jumuiya hiyo ni muhimu katika kusimamia malezi na maadili ya viongozi wa chama na jumuiya zake hivyo kuwa na uwezo wa kiuchumi kugharamia shughuli zake itaondoa unyonge kuwa omba omba kila wakati.
![]() |
Awali katibu wa CCM wilaya Kigoma Vijijini, Rashidi Semindu Pawa alisema kuwa mwaka huu na mwaka ujao ni miaka ya uchaguzi hivyo Pamoja na majukumu mengine viongozi na wanachama wa jumuiya hiyo wanalo jukumu kubwa la kusimama imara katika kuhakikisha ushindi wa viongozi watakaopitishwa na chama kwenye chaguzi zinazokuja.
Semindu Pawa alisema kuwa katika chaguzi hizo jumuiya hiyo inalo jukumu kubwa la kuwaibua wagombea ambao wamelelewa na kupata malezi kupitia jumuiya za chama ili wawe viongozi wenye utashi katika kusimamia maendeleo na matatizo ya wananchi.
Akizungumza katika mkutano huo Padre Simon Madata ambaye alikuwa ni miongoni mwa viongozi wa madhehebu mbalimbali ya dini waliolalikwa kwenye mkutano huo ametaka siasa itawaliwe na haki na amani ili kuwapa nafasi sawa wagombea waweze kutumia vizuri nafasi zao kuwatumikia wananchi.
0 Comments