Header Ads Widget

MAHAKAMA YA TAIFISHA V8 ILIYOSAFIRISHA WA WAHAMIAJI HARAMU KWA NAMBA ZA SERIKALI



Mahakama ya Wilaya ya Babati Mkoani Manyara imelitaifisha na kuwa mali ya Serikali, gari aina ya Toyota Land Cruiser V8 lilikuwa na namba za serikali za STL, lililokamatwa likiwa limebeba Wahamiaji 17 Raia wa Ethiopia waliongia nchini bila kibali.

 

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Babati, Juma Mwambago, ikiongozwa na Mwendesha mashtaka Mkaguzi wa Uhamiaji Yohana Malima Machunde, akisaidiana na Mawakili wa Serikali ambapo pia Washtakiwa hao wamehukumiwa kulipa faini ya shilingi laki tano Kila mmoja au kwenda Jela miaka miwili.

 

Hata hivyo, raia 17 kutoka Ethiopia, wamehukumiwa kwenda Jela miaka miwili Kila mmoja baada ya kushindwa kulipa faini ya shilingi laki tano kwa Kila mmoja.

 

Gari hilo pamoja na Wahamiaji 17 lilikamatwa April 7, 2024 katika eneo la Kiongozi Babati baada ya Dereva kutelekeza gari hilo, alipobaini anafuatiliwa na Polisi baada ya kugoma kusimama katika kizuizi cha Minjingu.

 

Hii inakuwa ni V8 ya pili kukamatwa ikiwa na Wahamiaji wasiokuwa na vibali, Mkoani Manyara na kutaifishwa kuwa mali ya Serikali huku Wahamiaji hao wakihukumiwa kwenda Jela ambapo V8 ya kwanza ilikamatwa March 23 ikiwa na Bendera ya CCM huku ndani ikiwa na Wahamiaji haramu 20 Raia wa Ethiopia na siku chache baadaye ikataifishwa na Mahakama.

 

Itakumbukwa April 12,2024 Mahakama ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa pia ililitaifisha kuwa mali ya Serikali, gari aina ya Toyota LandCruiser V8 lililokamatwa likiwa limebeba Wahamiaji 16 Raia wa Ethiopia April 6,2024 katika eneo la Msitu wa Luganga kata ya Sao Hill, Mafinga Wilayani Mufindi.

 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS